Afisa Bidhaa wa NMB Adamu Karazani akibonyeza kitufe kuwapata washindi wa promosheni ya Ki-College zaidi na NMB. Kutoka (kushoto) ni Mkaguzi wa bodi ya michezo ya kubahatisha ya Taifa, Bakari Maggid (L) Selcom representative, Mwakilishi wa selcom Julio Batalio and Meneja Mawasiliano wa NMB, Josephine Kulwa.
Oktoba
1, 2012 NMB ilizindua promosheni ya Ki-COLLEGE zaidi na NMB
inayowawezesha wanafunzi wenye akaunti ya NMB Student Account kupata
nafasi ya kuingia kwenye droo na kujishindia zawadi mbalimbali kama:
iPad, Samsung Galaxy, Amana maradufu, flash disk, fulana za NMB, taa
inayotumia mionzi ya jua. Hivyo basi, wanafunzi waliofungua NMB Student
Account, walioweka amana katika akaunti zao au kujiungana NMB mobile
wameweza kuingia kwenye droo na wamepata nafasi ya kujishindia zawadi
kwenye promosheni ya Ki COLLEGE zaidi na NMB.
Katika
droo ya mwisho iliyochezeshwa Januari 7,2013 washindi 73 wamejishindia
zawadi mbali mbali ikiwemo; Ipad 1, Samsung Galaxy 1, Amana maradufu 1 ,
taa inayotumia mionzi ya jua 10, flash disk 50 na jezi za timu ya Taifa
10.
Pamoja na kampeni hii, wanafunzi walioofungua NMB Student Account wataendelea kufurahia huduma za NMB Student Account kama: kujiunga na huduma ya NMB mobile bure kupata huduma ya ujumbe mfupi kila utoapo fedha kwenye ATM ya NMB bure, kuchukua fedha hadi Sh.1,000,000 kwenye NMB ATM kwa siku na kupata huduma kupitia matawi zaidi ya 143 na NMB ATM zaidi ya 450 nchi nzima.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)