WANANCHI WATAKIWA KUTOJICHUKULIA SHERIA MIKONONI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WANANCHI WATAKIWA KUTOJICHUKULIA SHERIA MIKONONI

Mahmoud Ahmad Arusha

Wananchi wenye hasira kali hapa nchini wametakiwa kuacha kujichukulia sheria mikononi na kuwapiga ama kuwachoma moto watu wanaodaiwa kuwa ni wezi bila ya kujua kama madai wanaotuhumiwa nayo ni ya kweli au la na wengine kujikuta wakipoteza maisha bila ya kuwa na hatia na kutakiwa kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria na usalama.

Kauli hiyo imetolewa na wananchi mbali mbali wakati wakiongea na waandishi wa habari kwenye matukio mawili tofauti yaliyotoke kwenye sehemu mbili tofauti kwenye stand kuu ya mabasi na stand ndogo ya vifodi jijini hapa jana.

Katika tukio la kwanza kijana anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 37 mkazi wa jijini hapa mwenye ugonjwa wa akili alipata mkong'oto wa kufa mtu baada ya kupiga gari la mtu lililokuwa kwenye stand hiyo na kumwaga vyakula na karanga za wafanyabiashara ndogo ndogo na vijana stand hapo kumpa mkong'oto huo.

Vijana hao huku wakimpa mkong'oto kijana huyo walikuwa wakimwambia kuwa wanampa dawa ya sigareti kubwa kwani dawa yake wanayo wao kijana huyo aliendelea kupatiwa mkong'oto nhadi askari wa jeshi la polisi aliyekuwa doria stand hapo kumuokoa na kumfikisha kwenye vyombo vya usalama kumuokoa na kipigo hicho kutoka kwa vijana wasio na chembe hata ya huruma kwa mgonjwa huyo.

Katika tukio la pili kijana anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 17 mkazi wa jiji hili alipata mkong'oto wa paka mwizi hadi kushindwa kujua uelekeo wake wa kwenda baada ya kudai kuiba vitu kwenye duka moja stand ndogo ya vifodi.
 
Waandishi walipohoji kwa mwenye duka hilo ni vitu gani vimeibiwa kwenye duka hilo alishindwa kuthibitisha kuwa alIIbiwa nini dukani humo huku mgambo wa jiji wakiangali bila ya kuchukuwa hatua yeyote.

Tarifa zinadai kuwa wananchi mbali mbali wamekuwa wakipatiwa mkong'oto bila ya kuwa na hatia ya makosa wanayotuhumiwa na kuwataka wananchi mbali mbali kutokujichukulia sheria mikononi

Alipohojiwa kamanda wa polisi mkoani hapa Liberatus Sabas kuhusiana na wananchi kujichukulia sheria mkononi alisema matukio mengi ya kujichukulia sheria mkononi ni tatizo hapa nchini huku akiwataka watanzania kujenga mazoea ya kujichunguza kabla  ya kujichukulia sheria mkononi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages