Mratibu wa FAO Ofisi ya Zanzibar Ali
Haji Ramadhan akitoa hotuba ya makaribisho katika mkutano na waandishi
wa habari wa Visiwani Zanzibar ambapo amesema wanatarajia kupata mawazo
mengi zaidi ya kujenga kutoka kwa waandishi ambapo yatasaidia Umoja wa
Mataifa pamoja na Serikali kuihudumia nchi kwa upeo wa juu zaidi.
Mafunzo hayo ya siku moja yameandaliwa na Ofisi ya Mratibu Mkazi wa
Umoja wa Mataifa nchini kupitia timu ya wanawamasiliano wa UN.
Mwakilishi wa mratibu mkazi wa Umoja wa
Mataifa Zanzibar Anna Senga akizungumza na waandishi wa habari wa
visiwani Zanzibar kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo wao kama UN
katika kutekeleza hoja za mipango wa maendeleo (UNDAP) kutokana na
kuchelewa kupewa majibu na uchelewashaji wa utekelezaji wa mipango ya
maendeleo.
Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa
Tanzania Hoyce Temu akizungumza na waandishi wa habari wakati wa
mafunzo hayo ambapo ameelezea Mpango Mkakati wa UNDAP visiwani Zanzibar
ikiwemo kutoka ufafanuzi wa mafanikio pamoja na changamoto zinazoukabili
mpango huo.
Amesema mpango huu ni wa pamoja kwa
ajili ya Tanzania unaendena na mafanikio ya malengo ya maendeleo ya
kimataifa ambapo unachukua nafasi ya program za pamoja na miradi mingi
inayodhaminiwa na UN chini ya Model ya misaada ya maendeleo ya Umoja wa
Mataifa kwa mpango wa kazi moja ulioshikamana kwa ajili ya mifuko ya
fedha, program na wakala zote za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania.
Baadhi ya waandishi wa habari
waliohudhuria mafunzo hayo ya siku moja wakimsikiliza Afisa Mawasilano
wa Umoja wa Mataifa nchini Hoyce Temu.
Mmoja wa waandishi wa habari visiwani
Zanzibar akipitia makabrasha ya taarifa za utekezaji wa Mpango wa
Msaada wa maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDAP) zikionyesha nafasi ya UN
katika kuisaidia Serikali kwenye changamoto za maendeleo ya kibinadamu
zinazoikabili Tanzania wakati wa mafunzo hayo.
Pichani juu na chini baadhi ya waandishi
wa habari visiwani Zanzibar wakiuliza maswali kuhusiana na Mpango
Mkakati wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDAP) wakati wa mafunzo hayo.
Katibu wa Chama cha wanasheria wanawake
Zanzibar Hamisa Mmanga Makame akitoa somo katika mafunzo hayo ambapo
amezungumzia masuala ya Haki za Binadamu, umuhimu wa kuzingatia jinsia
na wajibu wa vyombo vya habari katika kuleta usawa.
Afisa Mipango mwandamizi wa shirika la
kazi duniani (ILO) Anthony Rutabanzibwa ambapo amevipongeza vyombo vya
habari vya Afrika Mashariki kwa kutoa kipaumbele katika habari
zinazohusu haki za binadamu na kuwataka waandishi kuzingatia zaidi
habari za kiuchunguzi ili kuwa na uhakika zaidi na yale wanayoaandika
ikwemo kujua chanzo cha habari unayoitoa.
Baadhi ya waandishi wa habari wa
visiwani Zanzibar wakiendelea kupigwa msasa juu ya shughuli za UNDAP na
masuala ya Haki za Binadamu kwenye mafunzo ya siku moja yaliyoandaliwa
na Ofisi ya Maratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini na kuendeshwa na
wanamawasiliano wa UN Tanzania.
Mwenyekiti wa UNCG Yusuph Al Amin
akielezea mada ya umuhimu wa mawasiliano kwa maendeleo na kuwataka
wamiliki wa vyombo vya habari na serikali kwa ujumla kubadilisha sera
zinazosimamia vyombo hiyo ili ziweze kutoa fursa kwa waandishi kuwa huru
katika uandishi na kuripoti habari bila kubanwa.
Meza Kuu Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa
Mawasiliano Ikulu Zanzibar Hassan Khatibu, Mratibu wa FAO Ofisi ya
Zanzibar Ali Haji Ramadhan, Mwakilishi wa mratibu mkazi wa Umoja wa
Mataifa Zanzibar Anna Senga, Mwezeshaji wa mafunzo hayo mwandishi
mkongwe Salim Said Salim na Mwenyekiti wa UNCG Yusuph Al Amin.
Rais wa Umoja wa vilabu vya waandishi
wa habari Kenneth Simbaya akitoa maoni yake kuhusiana na nini kifanyike
katika kuboresha tasnia ya habari ambapo ameshauri mafunzo kuendelea
kutolewa si tu kwa waandishi pia kwa wamiliki wa vyombo vya habari.
Pichani Juu na chini ni baadhi ya waandishi ws habari wa visiwani Zanzibar wakichangia mawazo yao wakati wa mafunzo hayo.
Afisa mipango wa Baraza la Habari Tanzania Ofisi ya Zanzibar Shifaa Said Hassan akichangia hoja wakati wa mafunzo hayo.
Sehemu ya waandishi wa habari
waliohudhuria mafunzo ya siku yaliyoandaliwa na Ofisi ya mratibu Mkazi
wa Umoja wa Mataifa Tanzania yaliyofanyka visiwani Zanzibar.
Afisa habari ngazi ya Taifa wa Kitengo
cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi.Usia Ledama (wa pili kushoto)
akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo.
Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akijadili jambo na wafanyakazi wenzake wakati wa mafunzo hayo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)