Wajumbe wa Sekretarieti ya
Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiongozwa na
Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana leo walitembelea na kukagua ujenzi wa Daraja la
Kikwete katika Mto Malagarasi lililopo wilayani Uvinza Mkoani Kigoma.
Ziara hiyo ya Wajumbe hao
ni moja ya shamra shamra za maadhimisho ya Miaka 36 ya CCM ambayo mwaka huu
inaadhimishwa Mkoani Kigoma kitaifa, na Wajumbe hao wameamua kukagua miradi
kadhaa ya Maendelea ambayo iliahidiwa na Chama hicho tawala wakati wa Kampeni
zake za Uchaguzi mwaka 2010.
Katika ziara hiyo Kinana
ameambatana na Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha Rose Migiro,
Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Katibu wa UVCCM taifa,Martin Shigela.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)