Nikiwa
nimesimama kulia katika picha hii pamoja na ujumbe wa Bodi ya Utalii
Tanzania TTB nje ya uwanja wa Klabu ya Sunderland kusini mwa Uingereza
mwezi Oktoba mwaka jana, Niliona mambo mengi ya kujifunza kama
watanzania ambayo kama tunataka kuyafikia inabidi tufanye uamuzi wa
kweli mioyoni mwetu ikiwa ni pamoja na matendo yetu Kifikra , Kitabia,
Kimaamuzi na kubadili mfumo wa utendaji kazi wetu wa kutothamini hata
sekunde moja inayopotea kila siku, Kuwa watu wa kujituma sana katika
kazi na kuheshimu utaratibu tuliojiwekea huku tukizingati kujifunza
zaidi katika Sayansi na teknolojia, bila kusahau matumizi ya fedha yenye
kuheshimu utaratibu wa kifedha na nidhamu ya hali ya juu, vinginevyo
tutabaki kuwa mabingwa wa kupanga mipango mezani na kwenye makaratasi
lakini utekelezaji unakuwa sifuri. Amka Mtanzania Jitambue la sivyo
tutabaki kuwa nyuma mpaka siku ya mwisho.
Hii
ni miongozi mwa Camera zaidi ya 24 zinazonasa matukio wakati wa michezo
ya mpira wa miguu katika ligi kuu ya Uingereza EPL katika kiwanja
kimoja matangazo ambayo hurushwa na mabingwa wa ulimwengu wa michezo
Televisheni ya SuperSport ya Afrika Kusini, wanastahili pongezi kwa kazi
nzuri wanayoifanya katika michezo ulimwenguni kote.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)