Jumatatu iliyopita tuliweza kuandika juu ya mawasiliano ya satelite ambao ndio mfumo wa digitali Somo ambalo linakujia kila Siku ya Jumatatu Saa Mbili na Nusu Hapahapa Lukaza Blog. Ni somo ambalo linakupa fursa ya kuelewa Juu ya MFumo mzima wa Mawasiliano ya Satelite na Masafa ya Mawimbi....
Tulipoishia Jumatatu Iliyopita Unaweza Kubofya Hapa..
Leo tunaendelea na Somo letu na Tutaangalia Juu ya Masafa ya Mawimbi ya Televisheni na redio Kutoka katika Mawasiliano ya Satelite
Masafa ya
Mawimbi ya Televisheni / Redio toka katika satelaiti (downlink
frequencies) katika eneo letu ITU Region 1 (Afrika, Ulaya, Uarabuni na
Urusi)
Mawasiliano ya Televisheni na Redio tunazozipokea toka katika satelaiti yapo katika "Electromagnetic Spectrum" kati ya 3GHz - 30GHz.
Kwa C Band masafa yanayotumika kutuma mawasiliano toka katika satelaiti hadi kwenye madishi tunayoyatumia ni 3.7GHz - 4.2GHz.
Kwa Ku Band masafa yanayotumika kutuma mawasiliano toka katika satelaiti hadi kwenye madishi tunayoyatumia ni 10.7GHz hadi 12.75GHz.
a) CHANELI ZA MULTICHOICE/ DSTV
Kutafuta chaneli za Multichoice/ Dstv kutoka katika satelaiti Eutelsat 36B iliyopo nyuzi za longitudo 35.9 (Mashariki mwa Mstari wa Greenwich) wanayoitumia kutupatia chaneli zao. Hii ni kwa sehemu ambazo satelaiti hii inafikisha mawimbi yake Tanzania ikiwa mojawapo.
Mawasiliano ya Televisheni na Redio tunazozipokea toka katika satelaiti yapo katika "Electromagnetic Spectrum" kati ya 3GHz - 30GHz.
Kwa C Band masafa yanayotumika kutuma mawasiliano toka katika satelaiti hadi kwenye madishi tunayoyatumia ni 3.7GHz - 4.2GHz.
Kwa Ku Band masafa yanayotumika kutuma mawasiliano toka katika satelaiti hadi kwenye madishi tunayoyatumia ni 10.7GHz hadi 12.75GHz.
a) CHANELI ZA MULTICHOICE/ DSTV
Kutafuta chaneli za Multichoice/ Dstv kutoka katika satelaiti Eutelsat 36B iliyopo nyuzi za longitudo 35.9 (Mashariki mwa Mstari wa Greenwich) wanayoitumia kutupatia chaneli zao. Hii ni kwa sehemu ambazo satelaiti hii inafikisha mawimbi yake Tanzania ikiwa mojawapo.
Eutelsat 36B iliyopo nyuzi za longitudo 35.9 Mashariki mwa mstari wa Greenwich.
Satelaiti hii iko wapi?
Satelaiti hii ipo katika nyuzi za longitudo 35.9°E Mashariki mwa Mstari wa Greenwich.
Ni satelaiti inayomilikiwa na kampuni ya Eutelsat; ilitengenezwa na Kampuni inayoitwa Thales Alenia Space
iliyopo katika bara la Ulaya (ina ofisi Ufaransa, Italia, Ubelgiji,
Hispania na Califonia - Marekani). Ilipelekwa angani na kuwekwa katika
obiti 36,485.7km toka ardhini (ipo katika nyuzi za longitudo 35.9°E) juu
ya Ikweta tarehe 24/11/2009 na kifaa kinachoitwa Proton Rocket. Muda
wake wa kutumika ikiwa angani ni miaka kumi na tano (miaka 15) maana
yake mwaka 2009 + miaka 15 = mwaka 2024. Kwa hiyo muda wa kuitumia
satelaiti hii ni hadi mwaka 2024. Eutelsat 36B imeambatanishwa na Eutelsat 36A ambayo ipo katika nyuzi za longitudo 36 Mashariki mwa mstari wa Greenwich (zilivyowekwa ni kama
satelaiti moja.). Ikiwa katika obiti yake inafikisha mawimbi yake
Afrika, Ulaya, Urusi, Maeneo ya Uarabuni na katikati ya bara la Asia.
Jedwali lililoko hapo chini linaonesha Masafa na Channel za Multichoice/ Dstv tunazozipokea nchini Tanzania na nchi nyingine ambazo Eutelsat 36B inafikisha mawimbi yake.
Haya masafa huwasaidia mafundi wakati wa kufunga madishi (kutafuta signal za Dstv).
Eneo katika bara la Afrika ambalo Eutelsat 36B inafikisha mawimbi yake "Eutelsat 36 B Footprints on Sub Saharan Beam"
Picha hapo juu inaonesha maeneo ambayo Eutelsat 36B inafikisha mawimbi
yake; pembeni ni kiwango cha mawimbi "signal power" toka katika
satelaiti (nguvu ya mawimbi haiko sawa kwa maeneo yote ambayo satelaiti
hii inafikisha mawimbi yake. Sehemu nyingine mawimbi yana nguvu sana na
sehemu nyingine nguvu ya mawimbi ni ya kawaida.
Eneo katika bara la Afrika ambalo Eutelsat 36B inafikisha mawimbi yake "Eutelsat 36 B Footprints on Central European Beam"
Eneo katika bara la Afrika ambalo Eutelsat 36B inafikisha mawimbi yake "Eutelsat 36 B Footprints on Eutelsat 36B Eurasia beam"
Eutelsat 36B Eurasia beam
Eneo katika bara la Afrika ambalo Eutelsat 36B inafikisha mawimbi yake "Eutelsat 36 B Footprints on Eutelsat 36B Russia beam"
Eneo katika bara la Afrika ambalo Eutelsat 36B inafikisha mawimbi
yake "Eutelsat 36 B Footprints on Eutelsat 36B Southern Africa beam"
Eutelsat 36B Southern Africa beam
Somo litaendelea Jumatatu ijayo Hapahapa Lukaza Blog Na Muda ni Uleule saa mbili na Nusu Asubuhi Tunakaribisha maswali ambapo tutamtumia Mtaalamu wetu Aweze kujibu. Unaweza Kututumia Maswali juu ya MAda hii.
Endelea Kuwa na Lukaza Blog 24/7 @ LUKAZA BLOG
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)