SOMO LETU LA 4 LEO JUMATATU: NINI SABABU KUBWA YA KUTUMA MAWIMBI KATIKA NJIA TOFAUTI TOFAUTI. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SOMO LETU LA 4 LEO JUMATATU: NINI SABABU KUBWA YA KUTUMA MAWIMBI KATIKA NJIA TOFAUTI TOFAUTI.

Habari za Mwisho wa Wiki. ni matumaini yetu kuwa Wiki yenu mliimaliza Njema na Mnaanza wiki nyingine mkiwa na Afya tele na Kwa wale ambao Wagonjwa Tunawaombea Kwa Mwenyezi Mungu Awaponye haraka ili Muweze kurejea katika kazi za ujenzi wa Taifa na Kujiongezea Kipato na Kuhakikisha tunapambana na Adui Mkubwa kabisa UMASKINI.
 
Jumatatu ya Wiki iliyopita tuliweza kuangalia juu ya vifaa vinavyotumika katika Kutafuta chaneli katika madishi na aina ya madishi ambayo unaweza kupata channel nyingi zaidi kama Ulikosa Somo Hilo la Jumatatu iliyopita Unaweza Kulipata Kwa  KUBOFYA HAPA

SOMO LETU LA LEO LINAANZA HAPA CHINI:

Nini sababu kubwa ya kutuma mawimbi katika njia tofauti tofauti? Namaanisha kwa nini Left Circular, Right Circular, Vertical na Horizontal?
Sababu kubwa ya kufanya hivi ni "Frequency Reuse" mawimbi ya masafa katika frequency moja mfano 3642MHz - Right Circular ni tofauti na 3642MHz - Left Circular hivyo frequency moja inaweza kutumika zaidi ya mara moja bila kuingiliana kwa kutenganishwa na "Polarity".

Vertical na Horizontal
Katika LNB kuna antena mbili; moja kwa ajili ya kuyapokea mawimbi ya vertical na nyingine kwa ajili ya mawimbi ya horizontal. Antena ya Vertical hupokea mawimbi ambayo ni Vertical na kuyapeleka katika sakiti ya Vertical na Antena ya Horizontal hupokea mawimbi ambayo ni Horizontal na kuyaeleka katika sakiti ya Horizantal.
 
Sakiti ya Horizontal hutumia umeme wa Voti 18V na sakiti ya Vertical hutumia Voti 13V. Umeme huu hutoka katika risiva. Kwa hiyo waya unaounganisha risiva na LNB hupeleka umeme wa voti 13V kwa sakiti ya vertical na voti 18V kwa sakiti ya Horizontal na vilevile hubeba mawimbi (Intermediate Frequency) kutoka katika LNB kwenda katika risiva.

Unapochukua rimoti ya risiva ya satelaiti na kuweka chaneli mfano; CAPITAL televisheni risiva hupeleka voti 13V katika LNB kwa sababu Capital Televisheni mawimbi yake ni Right Circular ambayo hubadilishwa na Teflon Slab kuwa Vertical. Ukichukua rimoti na kuweka chaneli ya Startv (Left Circular ambayo hubadilishwa na kuwa Horizontal) risiva hupeleka voti 18V katika LNB.

Kwa wanaounganisha risiva zaidi ya moja:
Kama tulivyoona hapo juu Vertical ni Voti 13V na Horizontal ni Voti 18V. Ukiunga risiva zaidi ya moja na kutumia LNB ambazo si "Single Solution" (LNB zenye uwezo wa kugawa mawimbi na kuyasambaza kwa risiva mbalimbali) kuna wakati baadhi ya chaneli zitagoma kuonekana.

Kwa nini baadhi ya chaneli zitagoma kuonekana?
Hii ni kwasababu katika risiva ya kwanza  mtu akichagua EATV (Right Circular - Vertical  = 13V) risiva yake itapeleka Voti 13V katika LNB, na mwingine akichagua TBC (Left Circular - Horizontal = 18V) risiva yake itapeleka Voti 18V katika LNB hiyohiyo. Hii huichanganya LNB na wakati mwingine risiva.
 
Ukitaka kuunganisha risiva zaidi ya moja hakikisha unatumia LNB ya output mbili, au zaidi ambazo output zake kila moja inajitegemea au tumia "Single Solution LNB" kwa C Band. Kwa Ku Band hutakiwa kutumia LNB ambayo ina output zaidi ya moja (kila output inajitegemea) au Quatro LNB.

Kinachofanyika katika LNB ya Ku Band.
Ndani ya LNB kuna antena mbili ndongo ambazo hupokea mawimbi ya satelaiti na kuyapeleka katika sakiti ambayo huyakuza (amplify) na kuyaelekeza katika hatua nyinginezo. Baada ya kuyakuza hupelekwa katika sakiti ambayo hutengeneza mawimbi karibia sawa na yale yaliyotoka katika satelaiti; sakiti hiyo tunaiita "local oscillator". Mawimbi yaliyotoka katika satelaiti katika Ku Band 10700MHz - 12750MHz huchanganywa na mawimbi yaliyotengenezwa na "LNB Local oscillator" ambayo ni Low Frequency 9750MHz na High Frequency 10700MHz.

Intermediate Frequency (IF):
LNB hufanya hesabu (computes) ya kuchukua mawimbi yaliyotoka katika satelaiti na kutoa yale iliyotengeneza yenyewe katika hatua tunayoiita "Heterodyning". Hata TV, Radio risiva nazo hufanya hatua hizi wakati wa kuandaa picha na sauti. Baada ya hesabu hiyo kinachopatikana ni Intermediate Frequency (IF).

Hesabu yenyewe:
Mawimbi yaliyotoka katika satelaiti katika Ku Band 10700MHz - 12750MHz.
Mawimbi yaliyotengenezwa na LNB ya Ku Band   -   9750MHz -  10700MHz.
Intermediate Frequency (IF)                                  =      950MHz    -  2050MHz
 
Kwa baadhi ya LNB za Ku Band:
Mawimbi yaliyotoka katika satelaiti katika Ku Band 10700MHz - 12750MHz.
Mawimbi yaliyotengenezwa na LNB ya Ku Band   -   9750MHz -  10600MHz.
Intermediate Frequency (IF)                                  =      950MHz    -  2150MHz


Hii inamaanisha kwamba mawimbi yanayopita katika waya kutoka kwenye LNB ya Ku Band kwenda katika risiva ni kati ya 950MHz hadi 2050MHz au 950MHz - 2150MHz. Mawimbi haya yanaweza kupita katika waya na ukitumia " spectrum analyzer" inayoweza kuona hadi 15GHz , 20GHz au 30GHz unaweza kuyaona na kuyachunguza.

ANGALIZO:
Intermediate Frequency (IF) kwa C Band inapatikana kwa hesabu ifuatayo:

C Band:
C-Band: IF frequency = local oscillator frequency - received frequency

Local Frequency ya C Band ni 5150MHz.

Mpangilio wa Masafa tunayoyatumia kupata chaneli za televisheni/ radio katika Ku Band kwa undani zaidi.
 
Umeme unaokwenda katika LNB toka katika Risiva
Sauti ya kuiamsha LNB (Tone)
LO (Low Frequency) Masafa ya chini  katika LNB
Ukaaji wa Mawimbi (Polarization)
Masafa yanayopokelewa
IF (Intermediate  Frequency)
13 V
0 kHz
9.75 GHz
Vertical
Low Band (10.70-11.70 GHz)
950-1950 MHz
18 V
0 kHz
9.75 GHz
Horizontal
Low Band (10.70-11.70 GHz)
950-1950 MHz
13 V
22 kHz
10.60 GHz
Vertical
High Band (11.70-12.75 GHz)
1100-2150 MHz
18 V
22 kHz
10.60 GHz
Horizontal
High Band (11.70-12.75 GHz)
1100-2150 MHz

Baadhi za LNB za Ku Band hufanyakazi kuanzia 10.7GHz hadi 12.75GHz na nyingine hufanya kazi kuanzia 10.6GHz hadi 12.75GHz. Katika satelaiti hii Eutelsat 36B Multichoice / DStv wapo wanatumia High Band (masafa wanayotumia yanaanzia 11.7270GHz – 12.245GHz).

Angalia jedwali hapo juu:
Vertical High Band      11.70GHz – 12.75GHz
Horizontal High Band 11.70GHz – 12.75GHz

Jambo muhimu:
Kadri masafa yanavyoongezeka ndivyo mawimbi yanavyokuwa rahisi kupotea katika waya. Katika masafa makubwa tunahitaji kutumia waya bora; vinginevyo mawimbi yanayofika katika risiva au decoder yanakuwa madogo (mawimbi hupotea njiani). Kwa lugha ya kitaalam tunasema "signal attenuation along cables". Waya tunaotumia kusafirisha mawimbi toka katika antena kwenda katika decoder za; mfano Startimes, Ting, Easy TV, au antenna zinazoungwa moja kwa moja katika televisheni zinaweza kushindwa kupitisha vizuri mawimbi kutoka katika LNB ya dishi kwenda katika risiva au decoder kama wavu wa waya unaouzunguka waya wa katikati wa"COAXIAL CABLE" hauna waya nyingi (if the coaxial cable shielding is not well brided).

Ku Band ipo ndani ya "Electromagnetic Spectrum - 3GHz hadi 30GHz" katika masafa ya 10.7GHz (10700MHz) hadi 12.75GHz (12750MHz) kutoka katika satelaiti (Ku band Television downlink frequencies).

Au setup mwenyewe kwa kubadilisha (edit katika risiva); LNB Frequencies za C Band ambazo ni 5150MHz na kuweka za Ku Band kama inavyoonekana hapa chini.

Satellite setup (katika risiva):
LNB Frequency
Low Frequency: 9750MHz
High Frequency: 10700MHz

Katika channel search (kila risiva ina MENU yake tofauti na nyingine):
Ingiza masafa (frequency), Symbol Rate na polarization (polarization weka Auto) katika jedwali ifuatayo (chagua mojawapo). Anza kutafuta signal. Ukishapata unganisha kila kitu sawa (weka waya vizuri) alafu unganisha decoder ya Multichoice/Dstv; utapata picha.

Mfano:

Ingiza katika risiva au decoder:
Frequency : 11785
Symbol Rate: 27500
Polarization: Horizontal
FEC (Forward Error Correction): ¾  au Auto

Mambo ya kuzingatia wakati wa kutafuta chaneli za Multichoice / DStv yanayotoka katika satelaiti Eutelsat 36B.
Baada ya kutafiti sana mawimbi ya satelaiti hii yanaonekana kuwa imara (stable) kwa frequency zote ila kuna tatizo linalojitokeza ni upande wa dishi.

Tatizo lenyewe:
Kutokana na sababu za kijiografia sisi (Tanzania) tupo jirani na satelaiti hii (inakuwa kama ipo utosini). Madishi yanayotumika kwa wingi kupokea chaneli za Multichoice/ DStv ni ya kipenyo cha sentimita 90(cm). Mara nyingi wakati wa mvua kwa wanaotumia madishi ya ukubwa huu lazima mawimbi yakatikekatike. Kwa sababu kadri masafa yanavyozidi kuongezeka katika "electromagnetic spectrum" unavyozidi kwenda juu; ("SOMA ELECTROMAGNETIC SPECTRUM") ndivyo yanavyozidi kuathiriwa na mvua. Ili kupata mawimbi ambayo hayakatiki hata wakati wa mvua tunahitaji kutumia madishi ya ukubwa wa sentimita 120(cm) ambayo ni sawa na mita 1.2(m).

Madishi mengi ya Ku Band yaliyopo sokoni (satellite dishes on the market) yanasumbua wakati wa kutafuta satelaiti hiyo kwasababu hayazunguki sana (vertical movement). Yanaishia pale satelaiti ilipo hivyo inakuwa vigumu kurekebisha vizuri ilikupata mawimbi vizuri. Pia stand zake (dish bases) zinazokuja na madishi hayo ni fupi kiasi kwamba ukizifunga ukutani madishi yanagusa ukutani. Hili ni tatizo lililopo katika utengenezaji wa madishi ya Ku Band na Multichoice/ Dstv inabidi tatizo hili walitazame kwasababu linawahusu. 
 
Somo litaendelea Jumatatu ijayo Hapahapa Lukaza Blog Na Muda ni Uleule saa mbili na Nusu Asubuhi Tunakaribisha maswali ambapo tutamtumia Mtaalamu wetu Aweze kujibu. Unaweza Kututumia Maswali juu ya MAda hii.
 
Endelea Kuwa na Lukaza Blog 24/7  @ LUKAZA BLOG

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages