regia mtema foundation yaandaa siku maalum ya kumbukumbu ya regia mtema. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

regia mtema foundation yaandaa siku maalum ya kumbukumbu ya regia mtema.

 Marehemu Regia Mtema enzi za uhai wake.

Siku ya Jumatatu; tarehe 14 January 2013 ni siku ambayo Regia Mtema Foundation imeitenga maalumu kwa ajili ya kumbukumbu ya Regia Mtema. Katika siku hii maalumu wote mnakaribishwa Peacock Hotel ambako kutakuwa na maada mbalimbali zitakazowasilishwa na kujadiliwa kama alivyozisimamia Regia. Katika siku hii maalumu wageni na wadau mbalimbali wamethibitisha kushiriki.

Hafla hii maalumu itaanza saa 9.00 Alasiri na kumalizika 2.00 usiku na kisha kufuatiwa na chakula cha usiku. Ratiba kamili itahusisha matukio yafuatayo:


1.      Historia ya Regia itakayowasilishwa na Mh. David Kafulila
2.      Mada juu ya Rushwa itakayowakilishwa na Takukuru
3.      Ulemavu Siyo Kutoweza itakayowasilishwa na Bi Shida Salum - Mwenyekiti CHAWATA

4.      Nafasi ya Kijana katika kuchochea maendeleo na demokrasia - Mh. January Makamba
5.      Majadiliano
6.      Documentary za Regia Mtema
7.      Remarks kutoka kwa Mh. Zitto Kabwe; Mh. John Mnyika na Hussein Bashe na Mzee Mtema

8.      Chakula cha jioni
9.      Networking

Wasimamizi wa hafla hii watakuwa: Pascal Mayalla na Lara Williams

Thibitisha kuhudhuria kwako kwako kupitia number: 0713 694 820
RMF inawaomba Wanahabari wote wasaidie kusambaza mwaliko huu.

Wasalaam

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages