Mvua
kubwa iliyonyesha mapema leo mjini Mtwara imepelekea mafuriko katika
maeneo mbali mbali ya mji huu na kufanya wakazi wa maeneo haya kupata
kuanza kuhangaika kuhamisha vitu vyao na wengine wakiwa hawajui la
kufanya maana maji yamejaa mpaka majumbani mwao.Ni balaa kubwa la
mafuriko ya maji Mtwara leo hasa eneo la Chuno. Eneo hili ni karibu na
nyumba ya Mzee Hokororo au Dr Mwakipa. Hali ni mbaya sana na maji
yanaendelea kujaa hadi mchana huu.Hakuna taarifa yeyote mtu yeyote
aliyepoteza maisha. Msaada wa haraka unahitajika kwa wananchi hawa.Picha
na Mdau Abdulaziz Video
-
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)