Wanachama
wa timu ya Yanga kutoka sehemu mbalimbali wakitawanyika nje ya jengo la
bwalo la Maofisa wa Polisi,Oysterbay jijini Dar mapema leo mchana mara
baada ya kumalizika mkutano wao mkuu wa Mwaka,ambao kwa hakika
umefanikiwa kwa kiasi kikubwa,Mkutano huo uliratibiwa na kampuni ya
Prime Time Promotions Ltd ya jijini Dar na kurushwa Live kupitia Clouds
TV,aidha Mkutano huo ulionekana kunoga zaidi kufuatia timu hiyo ya Yanga
kuifumua timu ya Black Leopards ya nchini Afrika kusini katika mechi
yao ya kirafiki iliyofanyika hapo jana kwenye Uwanja wa Taifa bao 3-2.
Mwenyekiti
Mpya wa Club ya Yanga Africans,Yusuf Manji akifafanua mambo mbalimbali
kwenye mkutano huo,uliochanganua mambo mbalimbali zikiwemo changamoto za
timu hiyo,maendeleo yao mbalimbali ikiwemo samabamba na ujenzi wa
kiwanja kikubwa cha mpira maeneo ya Jangwani,jijini dar,Sahihisho la
katiba yao,masuala mbalimbali ya yanayohusiana na wanachama wao,ustawi
wa wanachama wao,mikataba baina yao na wadhamini wao na mambo mengine
mbalimbali.
Sehemu ya meza kuu ya mkutano huo ilivyokuwa.
Makamu mwenyekiti wa timu ya Yanga,Clement Sanga akitolea ufafanuzi moja ya jambo lililoulizwa na wajumbe wa mkutano huo.
Pichani
kulia ni mchezaji wa timu ya Yanga,Shadrack Nsajigwa akipeana mkono wa
shukurani na Mwenyekiti wa Yanga,Yusuf Manji mara baada ya kutajwa kuwa
ndiye mchezaji aliyedumu Yanga kwa muda mrefu miongoni mwa wachezaji
waliopo hivi sasa,hivyo alizawadiwa barua ya shukurani na kitita cha
shilingi milioni moja.
Pichani
juu na chini ni baadhi ya Wajumbe wa timu ya Yanga waliopata nafasi ya
kuuliza maswali mbalimbali kwa Kamati ya Utendaji,mbele ya wageni
waalikwa mbalimbali waliohudhuria mkutano huo.
Mwenyekiti
wa Yanga,Yusuf Manji sambamba na Makamu mwenyekiti wa timu hiyo,Clement
Sanga wakifatilia jambo kwa makini ukumbini humo.
Pichani baadhi ya wachezaji wa timu ya Yanga pia walihudhuria mkutano huo uliohusu mikakati mbalimbali ya kuimarisha timu hiyo.
Baadhi ya Wazee wa baraza wa timu ya Yanga wakifautilia kwa makini yaliyokuwa yakijili kwenye mkutano huo mkuu wa Kihistoria.
Kocha
mpya wa timu ya Yanga,kutoka nchini Uholanzi Ernest Brandts nae
aliruhusiwa kutoa yake machache kuhusina na timu yake ya Yanga.
Pichani
ni baadhi ya Wanachama wa Yanga waliofurika kwa wingi ndani ya mkutano
mkuu wa timu hiyo uliofanyika ndani ya bwalo la Maofisa wa
Polisi,Oysterbay jijini Dar es salaam mapema leo asubuhi na kumalizika
mapema jioni ya leo.
Msanii mahiri wa kizazi kipya sambamba na wasanii wenzake kutoka THT wakitumbuiza kwenye mkutano huo.
Mtangazaji
machachari wa kipindi cha michezo,Clouds FM/TV Mbwiga Mbwiguke
akiwaweka sawa wanachama wa Yanga waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano
wao mkuu wa Mwaka.Picha Kwa Hisani ya Full Shangwe Blog
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)