Meneja
Masoko wa kampuni ya Car and General, Jonathani Masanja(pili kishoto)
akimuonesha Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf mwenda (kulia) pikipiki
ya miguu mitatu aina ya TVS KINGS itakayotolewa kwa mshindi wa kwanza
wa mashindano ya Meya Cup 2013. Kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni
hiyo Venkatesh Jayaraman, Hafla hii ya utambulisho wa mdhamini mwingine
wa Mashindano haya ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. NMB ikiwa ni
mdhamini Mkuu wa Mashindano hayo.
Meya
wa manisapaa ya kinondoni, Yusuph Mwenda akiiendesha pikipiki ya miguu
mitatu itakayokabidhiwa kwa mabingwa wa Kinondoni Meya Cup 2013 katika
mashindano yanayoshilikisha Mitaa zaidi ya 78 katika Wilaya ya
Kinondoni
………………………………………………………..
NMB inawawezesha wateja wake
kufanya biashara kiurahisi zaidi. katika hilo NMB imeungana na kampuni
inayosambaza pikipiki za miguu mitatu zinazojulikana kama TVS
KING.katika kuhakikisha kua kila mteja anakua na usafiri utakaomsaidia
kurahisiha au kuongeza kipato chake NMB imechukua jukumu la kutoa mikopo
kwa wateja wake ambapo mteja atatoa asilimia 30 kwanza ya gharama za
pikipiki hiyo ya miguu mitatu yenye thamani ya shilling milioni tano
laki sita tu.
Wilaya ya Kinondoni imeandaa
mashindano ya mpira wa miguu ambayo wameayaita Meya Cup 2013 na NMB ni
wadhimini wakubwa wamashindano hayo moja ya zawadi zitakazo tolewa kwa
mshindi wa kwanza ni TVS KING.
Akizungumza katika hafla hiyo
Jonathani Masanja, meneja masoko wa TVS KING amesema kwamba zawadi hiyo
itaisadia timu husika kujipatia kipato kwani inafaa katika biashara.na kwamba kama vijana wakilijua hilo wataweza kujiajiri kwa kupitia TVS KING
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)