Makamu
wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athuman Jumanne Nyamlaniakionyesha fomu
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athuman Jumanne Nyamlani akizungumza na
waandishi wa habari baada ya kuchukua katika ofisi za Shirikisho la Soka
Tanzania leo asubuhi.Picha na Dande Francis
---
Wadau
watatu wa mpira wa miguu wamechukua fomu za kuwania urais wa Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kufanya idadi ya waliojitosa katika
uchaguzi huo utakaofanyika Februari 24 mwaka huu kufikia 30.
Hata
hivyo, idadi hiyo ni kwa wale wanaochukua fomu hizo katika ofisi za
TFF, kwani vilevile zinapatikana kupitia tovuti ya TFF ya www.tff.or.tz ambapo mwisho wa kuchukua na kurejesha ni saa 10 kamili alasiri Januari 18 mwaka huu.
Waliochukua
leo (Januari 16 mwaka huu) kuwania urais ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa
TFF, Athuman Jumanne Nyamlani, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu
Mkoa wa Kagera (KRFA), Jamal Emil Malinzi na Mwenyekiti wa Chama cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa Kigoma, Omari Mussa Nkwarulo.
Mwengine
aliyechukua leo ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya
(MREFA), Elias Mwanjala anayewania ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF
kuwakilisha Kanda ya Iringa na Mbeya.
Orodha
kamili ya wadau waliochukua fomu kwenye ofisi za TFF ni Athuman Jumanne
Nyamlani, Jamal Emil Malinzi na Omari Mussa Nkwarulo (urais), Michael
Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia (umakamu wa rais).
Kwa
upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji na kanda zao kwenye mabano ni
Salum Chama (Kagera na Geita), Mugisha Galibona, Samuel Nyalla, Titus
Osoro na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza).
Epaphra
Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo na Elly
Mbise (Arusha na Manyara), Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu
Nyaulingo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na
James Mhagama (Njombe na Ruvuma).
Athuman
Kambi (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na
Singida), Farid Nahdi na Twahili Njoki (Morogoro na Pwani), Elias
Mwanjala (Iringa na Mbeya), Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga) na
Muhsin Balhabou, Shaffih Dauda na Zafarani Damoder (Dar es Salaam).
Kwa
upande wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) waliochukua fomu kwenye ofisi za
TFF mpaka sasa ni wawili tu. Yusuf Manji amechukua fomu ya uenyekiti
wakati Said Mohamed amechukua fomu ya kuwania umakamu mwenyekiti.
WAHARIRI, WAANDISHI WAPIGWA MSASA KANUNI ZA UCHAGUZI
Wahariri
na Waandishi wa Habari zaidi ya 40 wameshiriki kwenye semina kuhusu
Kanuni za Uchaguzi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
iliyofanyika leo (Januari 16 mwaka huu).
Wawezeshaji
katika semina hiyo iliyofanyika ofisi za TFF walikuwa Kamati ya
Uchaguzi ya TFF iliyoongozwa na Mwenyekiti wake Deogratias Lyato na
Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)