Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara
(kushoto) akiangalia mtambo wa kurushia matangazo ya redio kwa masafa
mafupi (Short Wave) na Televisheni wa Shirika la Habari la Tanzania
(TBC) hivi karibuni uliopo eneo la Nyashana jijini Mwanza. Kulia ni
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana James Kajugusi.
Mhandisi
Zablon Mafuru (kulia) ambaye ni mkuu wa Kituo cha Shirika la Utangazaji
Tanzania (TBC) Mwanza akimuonyesha Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kulia) hivi karibuni mtambo wa redio
Tanzania wa masafa marefu (Medium Wave) unaorusha matangazo yake katika
mikoa ya Mwanza, Geita, Mara, Shinyanga, Kigoma , Siminyu na nchi
jirani za Uganda na Rwanda uliopo Ilemela jijini Mwanza.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara
(kushoto) akikagua hivi karibuni kiwanja cha Shirika la Habari la
Tanzania (TBC) kilichopo eneo la Kapripointi jijini Mwanza. Kulia ni
Eston Sanga ambaye ni Mkuu wa Kanda ya Ziwa wa Shirika hilo.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (wa pili
kulia) akiongea jambo hivi karibuni na baadhi ya wafanyakazi wa
Shirika la Habari la Tanzanzani (TBC) mara baada ya kumaliza ziara yake
fupi ya kutembelea ofisi za kanda ya Ziwa za shirika hilo zilizopo
jijini Mwanza. Kulia ni Eston Sanga ambaye ni Mkuu wa Kanda ya Ziwa wa
Shirika hilo na wapili kushoto ni Mhandisi Zablon Mafuru ambaye ni mkuu
wa Kituo cha Mwanza akifuatiwa na Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya
Maendeleo ya Vijana James Kajugusi (aliyevaa suti ya dark blue).
Mhandisi
Zablon Mafuru (kulia) ambaye ni mkuu wa Kituo cha Shirika la Utangazaji
Tanzania (TBC) akimuonyesha Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Dk. Fenella Mukangara (wa pili kulia) mtambo wa kurusha
matangazo Televisheni kwa njia ya digitali (haupo pichani) uliopo eneo
la Nyashana jijini Mwanza. Kuanzia tarehe moja mwezi wa kwanza mwaka
2013 vituo vyote vya Televisheni vitarusha matangazo yake kwa njia ya
digitali. Picha na Anna Nkinda – Maelezo
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)