Mhe. Balozi Bertha Semu Somi, Mkurugenzi wa Masuala ya Diaspora akimfafanulia jambo Prof. Msafiri Mbaga ambaye ni Mtanzania anayeishi na kufundisha nchini Oman.
Sehemu ya Watanzania waishio Oman wakishiriki ufunguzi wa Mkutano.
Bw. Twisa Mwambona, Meneja wa Azania Bank akizungumza na Meneja wa Masuala ya Credit na Risk wa Bank of Oman.
Kamishna wa Hazina(Kulia) akitoa maelezo ya ufafanuzi wa Diaspora kuhusu Sheria za Fedha na Kodi nchini Tanzania. Katikati ni wadau kutoka Wizara ya Uchukuzi.
Bi. Josephine Kimarowa Menejimenti ya Utumishi wa Umma (katikati) na Bw. Joseph Haule wa Wakala wa Ajira(Kulia) wakizungumza na mdau aliyetaka kufahamu kuhusu fursa za huduma za Ajira na Utafiti (Consultancy) nchini Tanzania.
Bw. Hassan Hafidh kutoka Afisi ya Rais-Diaspora Zanzibar akizungumza na wadau wa Diapsora juu ya mipango ya Serikali ya Mapinduzi wa Zanzibar kwa Watanzania wenye asili ya Zanzibar waishio nje.
Bi. Patricia Nguma kutoka BOA Bank(kulia) akijadiliana na Mdau wa Diaspora kuhusu mikopo ya nyumb ya BOA.
Bw. Boniface Ngowi wa Wizara ya Viwanda na Biashara akitoa maelezo kwa Watanzania waishio Oman kuhusu Sera za Biashara nchini Tanzania.
Ujumbe wa Tanzania
unaoongozwa na Balozi Bertha Semu-Somi, Mkurugenzi wa Masuala ya
Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na
unajumuisha wajumbe kutoka Wizara za Mambo ya Nje, Fedha, Viwanda na
Biashara, Nishati na Madini, Menejimenti ya Utumishi wa Umma,
Miundombinu, Habari na Utamaduni, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu,Afisi ya Rais inayoshughulikia masuala ya Diaspora
Zanzibar na Tume ya Mipango Zanzibar.Aidha, ujumbe umehusisha Taasisi za Serikali za TBC,TIC,TCRA, EPZA, ZIPA, UHAMIAJI, TTB,TANAPA na Dar es Salaam Maritime Institute.
Ujumbe huu umejumuisha pia wajumbe kutoka Sekta Binafsi zikiwemo TPSF, BOA, Azania Bank, CRDB, PBZ, Uhuru One, Zanzibar Issurance Corporation na Zanzibar Chamber of Commerce.
Mkutano wa Diaspora umeitishwa kufuatia maazimio yaliyofikiwa katika Mkutano uliopita kati ya Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Watanzania waishio Oman ambapo aliwashawishi kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa Tanzania.
Mhe. Rais aliwaahidi kutuma timu ya wataalamu kukutana na Diaspora kuwajulisha juu ya fursa zilizoko nchini na kupokea changamoto zao zinazowakwamisha kuchangia katika uchumi wa Tanzania.
Katika kikao hicho kilichomalizika leo, watanzania waishio Oman wamepata fursa ya kukutanishwa na taasisi za Tanzania na kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali ikiwemo kuanzisha mawasiliano yenye lengo la kukuza ushirikiano wa kibiashara. Masuala yaliyojitokeza ni pamoja na haja ya kuanzishwa kwa Chama cha Watanzania waishio Oman.
Oman ni nchi ambayo wananchi wake wengi wana asili ya Tanzania kutokana na uhusiano wa kihistoria baina ya nchi hizi mbili. Inakadiriwa kuwa familia 780 za Watanzania wanaishi nchini Oman na kuendesha shughuli zao katika sekta binafsi na Serikali.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)