Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mkuu, Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mary Kidima wakatika
alipokagua banda la Taasisi hiyo katika maadhimisho ya Siku ya Haki za
Binadamu na Siku ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa yaliyofanyika kwenye
viwanja vya Mnazimmoja jijini Dar es salaam Desemba 10,2012.
Baadhi ya waandamanaji wakiandamana katika maadhimisho ya siku ya
haki za Binadamu na siku ya kuzuia Rushwa yaliyofanyika kwenye viwanja
vya Mnanzimmoja jijni Dar es salaam Desemba 10, 2012.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiongozana na Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias
Chikawe (wapili kulia), Naibu wake Angellah Kairuki (kulia),
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema (kushoto) na Mwenyekiti
wa Tume ya haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Mstaafu, Amir Maneto
(katikati) baada ya kuhutubia katika maadhimisho ya siku ya Haki za
Binadamu na Siku ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwenye viwanja vya
Mnazimmoja jijini Dar es salaam Desemba 10, 2012. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)