Mwadishi Mashuhuri wa Makala mbalimbali na habari za Kimahakama Happiness Katabazi(Kulia)akiwa na 'mkwe
wake 'ACP-Abdallah Zombe leo asubuhi katika Mahakama ya Rufaa Dar es
Salaam, muda mfupi baada ya rufaa iliyokatwa na DPP-Dk.Elezer Feleshi
kupinga hukumu ya kesi ya mauaji ya watu wanne dhidi ya Zombe na wenzake
kushindwa kusikilizwa na mahakama hiyo kwasababu jaji mmoja kati ya
majaji watatu wanaosilikiza kesi hiyo anaumwa.
Wakili Mwandamizi wa Serikali Angaza Mwipopo akisalimiana ACP-Abdallah Zombe leo asuhubi ndani ya Mahakama ya Rufaa
Hii ndiyo timu ya mawakili waandamizi wa serikali katika rufaa ya Zombe Timoth Vitalis, Edwin Kakolaki,Angaza Mwipopo,Prudence
Rweyongeza,Alexander Mzikilia,Mgaya Mtaki na Peter Njike, wakiwa ndani
ya ukumbi wa mahakama ya rufaa Dar es Salaam, lakini hata hivyo rufaa
hiyo haikuweza kusikilizwa kwasababu jaji mmoja anayeunda jopo la majaji
wa tatu anaumwa.
Zombe na
wakili wake Richard Rweyongeza.Na upande wa jamhuri unawakilishwa na
timu ya mawakili waandamizi wa serikali saba.Picha na Happiness Katabazi
--
Na Happiness Katabazi
MAHAKAMA ya Rufaa Dar es Salaam, jana ilishindwa kuanza kusikiliza rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP), Dk.Eliezer Feleshi dhidi ya aliyekuwa M kuu wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi(ACP),Abdallah Zombe na wenzake kwasababu jaji mmoja ambaye anaunda jopo la majaji wa tatu Semistocles Kaijage anaumwa.
DPP.Feleshi anapinga hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es
Salaam na Jaji Salum Massati ambaye kwasasa ni jaji wa mahakama ya rufaa kwasababu hukumu ile ina makosa ya kisheria na kwamba
jaji Masati akupaswa kuwaachilia huru wajibu rufaa hao na Jaji Natalia
Kimaro ndiyo aliarisha rufaa hiyo leo asubuhi na kuzieleza pande zote
mbili kuwa tarehe ya kuja kusikilizwa rufaa hiyo watapatiwa kwa
maandishi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)