Mkurugenzi
wa Maisha Plus Masoud Kipanya akizungumzia sakata hilo ambapo amesema
Maisha Plus mbali ya kazi yake ya kawaida kama shindano, lakini
imemkutanisha Ibrahim na ndugu zake na akasema kumbukumbu za picha
zimetusaidia kujua ukweli wa jambo lenyewe kuhusu sakata la Ibrahim.
Ibrahim alirudi nchini kwa
kumfuata rafiki yake hakumtaja jina ambaye inadaiwa ni mkenya wakawa
wanaishi mkoani Arusha, na ndipo alipofanikiwa kuingia katika kuwania
nafasi ya kushiriki katika Shindano la Maisha Plus, hata hivyo
hakufanikiwa kupita katika mchujo huo.
Mama mkubwa wa Ibrahim
alimfananisha Ibrahim na mshindi wa pili wa Maisha Plus Venance Mushi
ambaye ukiangalia kwa kiasi wanafanana, kutokana na historia aliyoitoa
Ibrahim jambo lililompa mashaka kwani mdogo wake Hedinesta aliwahi kuwa
na mimba lakini haikujulikana kilitokea nini mara baada ya kukimbia
nyumbani kwao Arusha na kwenda kwa dada yake huko mpakani mwa kenya na
Tanzania ambako inadaiwa alijifungua na baada ya mwezi mmoja
akumtelekeza mtoto huyo, aliyeshika kipaza sauti ni Emanuel Anderson
ndugu yake na Ibrahim





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)