Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akitoa hotuba ya ufunguzi wa jengo la ghorofa kwa ajili ya makazi ya Askari Magereza mjini Iringa. Ufunguzi huo uliambatana na sherehe kubwa ambayo iliudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na maofisa wa Jeshi la Magereza. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini CGP John Minja
Bila kujali mvua kubwa inayonyesha, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akiukata utepe akiashiria ufunguzi wa jengo la ghorofa kwa ajili ya makazi ya Askari Magereza mjini Iringa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (aliye vaa kiraia kushoto) akifunua kitambaa kuashiria ufunguzi wa jengo la ghorofa kwa ajili ya makazi ya Askari Magereza mjini Iringa. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini CGP John Minja.
Baadhi ya sehemu ya nje na ndani ya jengo hilo pamoja na maafisa mbalimbali wa jeshi hilo wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya jengo hilo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akipata maelezo wakati alipotembelea vyumba vya jengo hilo
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini CGP John Minja katika picha ya pamoja na maafisa waandamizi wa jeshi hilo baada ya ufunguzi wa jengo. PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA
SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)