Mti
huu kivuli chake ni ofisi ya walimu (staff room) wa Shule ya Msingi
Silabu iliyopo Wilaya ya Korogwe. Thehabari.com imelazimika kuitembelea
tena shule hii ikiwa ni miezi sita baada ya kuitembelea awali mapema
mwezi Agosti 2012.
Hili
ni darasa jipya lililojengwa sasa katika Shule ya Msingi Silabu iliyopo
Wilaya ya Korogwe, darasa hili linatumiwa na wanafunzi wa darasa la
tatu. Lakini nje kivuli chake wakati wa jua kali ni ofisi ya walimu wa
shule hiyo.
Madawati
haya mbele ya darasa hili ni Ofisi ya walimu (staff room) katika Shule
ya Msingi Silabu, husogezwa hapa baada ya kivuli cha mti kutoweka katika
mti ambao hutumika kama ofisi shileni hapo.
Uchochoro
huu awali ndio ulitumika kama darasa la tatu kwa wanafunzi wa Shule ya
Msingi Silabu iliyopo Wilaya ya Korogwe. Jitihada za Serikali zimefanywa
na sasa limejengwa darasa moja ambalo linatumiwa na wanafunzi wa darasa
la tatu. Thehabari.com imelazimika kuitembelea shule hii tena ikiwa ni
baada ya kipindi cha miezi sita. Awali (Agosti 2012) iliripoti wanafunzi
wa darasa la tatu kusomea uchochoroni baada ya kutokuwa na darasa.
Choo
hiki cha Shule ya Msingi Silabu kiliezuliwa na upepo muda mrefu sasa
lakini kutokana na hali ngumu ya bajeti ya fedha bado hakijarekebishwa,
Serikali inafanya juu chini kufanikisha hili itakapopata fungu la
kutosha.
TATIZO HILI NI NCHI NZIMA, SIJUI HAWA WAZEE WETU WALIO MADARAKANI WANAFIKIRIA NINI KUHUSU TAIFA LA BAADAE, KWA SABABU UKIJENGEA WATOTO MSINGI MBOVU WA ELIMU NA MAISHA BASI NA TAIFA LAKO HUKO BAADAE LITAKUWA BOVU. LABDA SERIKALI INAMPANGO WA KUTOA ELIMU BORA KWA WATU WACHACHE (WA FAMILIA ZAO BINAFSI ) ILI WAJIHAKIKISHIE KUTOKUSHTAKIWA KWA KUSABABISHA HALI HII NA KUENDELEZA KUJILIMBIKIZIA MALI NA KUACHA WATU WENGI MASKINI. WANASEMA "SISI TUMELALA WAO WANAISHI."
ReplyDelete