MKUU WA MKOA WA RUKWA AANZA ZIARA YA SIKU NANE KUHAMASISHA SHUGHULI ZA KILIMO MKOANI HUMO LEO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MKUU WA MKOA WA RUKWA AANZA ZIARA YA SIKU NANE KUHAMASISHA SHUGHULI ZA KILIMO MKOANI HUMO LEO


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akihutubia wananchi wa kata ya Matanga leo katika ziara yake ya siku 8 kwa ajili ya kuhamasisha shughuli za kilimo Mkoani Rukwa. Ziara hiyo itahusisha Wilaya zote tatu za Mkoa wa Rukwa ambazo ni Sumbawanga, Kalambo na Nkasi pamoja na
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akipokea maelezo ya shamba darasa kutoka Afisa Ugani Kata ya Matanga Ndugu Edith Shirima leo alipoanza ziara yake Mkoani Rukwa kwa kuanzia katika kata hiyo. Kulia ni Afisa kilimo Manispaa ya Sumbawanga Ndugu George Lupilya, Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Sumbawanga. Kushoto ni Katibu wa Mkuu huyo Mkoa Frank Mateni. 
Shamba darasa katika kata ya Matanga kijiji cha matanga linalomilikiwa na Mkulima mdogo Bibi Paschalia Ntinda. Mbolea ya kupandia iliyotumika ni Minjingu Mazao. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akisalimiana na Bibi Paschalia Ntinda amabaye ni mmiliki wa shamba darasa hilo.  
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kushoto akisalimiana na wananchi wakulima katika kata ya kasense leo alipoenda kukagua mashamba darasa katika kata hiyo. Kata ya Kasense ipo katika Manispaa ya Sumbawanga.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kulia akishiri katika palizi ya mahindi na kinamama wakulima wa kata ya Kasense leo akiwa ziarani katika kata hiyo kwa ajili ya kuhamasisha shughuli za kilimo Mkoani Rukwa. 
Ziara hii ya Mkuu wa Mkuu wa Mkoa inaenda sambamba na chanjo ya minyoo na vitamin A kwa watoto walio chini ya miaka mitano. Kwa kuunganisha zoezi hili na ziara yake kunatoa fursa kubwa kwa wananchi hususani wa vijijini kuwafikisha watoto wao kupata chanjo hizo kwa wingi na kirahisi. Katika kata ya Matanga yenye vijiji vitatu jumla ya watoto 86 walipatiwa chanjo hiyo.
Muuguzi Msaidizi Manispaa ya Sumbawanga Bi Shangwe Blaya akimpa mtoto Ezeckiel Chokola chanjo ya vitamin A katika kata ya Matanga ulipofanyika Mkutano kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na wananchi wa Kata hiyo leo. 

Halmashauri zake. Ziara yake inabeba ujumbe huu ufuatao:
1. Mkuu wa mkoa wa Rukwa anawatakia kila la kheri wananchi wote katika kusherekea sikukuu ya Noeli na Mwaka Mpya. Anawaomba kudumisha amani, Upendo na Mshikamano kwenye maeneo yetu na tupashane habari. Toa taarifa Polisi kwa jambo lolote lisilo la kawaida. Tuwatambue wageni wote wanaofika katika maeneo yetu wengine si watu wema.

2. Mkuu wa mkoa anawataka viongozi wote katika ngazi zote kuwajibika na kuwa waadilifu katika kutimiza wajibu wao.


3. Kila familia ihakikishe kuwa inatumia fursa hii ya msimu wa mvua katika kujiondoa na balaa la njaa na pia umaskini wa kipato. Viongozi wa kata na vijiji wafuatilie ili kujua kila kaya imelima kiasi gani katika msimu huu. Kila kijiji kiwe na Daftari la wakulima. Wakulima watashindanishwa.

4. Kila kijiji kitenge maeneo maalum kwa ajili ya kuendeleza shughuli maalum kama Ufugaji, kilimo na kuchague nguzo yake kuu ya uchumi. (Mpango wa SAGCOT).

5. Watoto wote watakaofaulumwaka huu wa 2012 lazima wapelekwe shule. Watoto wa kike wanastahili kulindwa ili wasipate ujauzito. Mzazi awe mlinzi namba moja.

6. Akina mama wapeleke watoto wao wa chini ya miaka mitano ili kupata chanjo ya minyoo na Vitamin A.

7. Kuanzia mwezi wa Januari 2013 watoto wa miezi 9 watapatiwa chanjo ya kuzuia kuharisha na Kichomi. Hivyo wazazi wote tuwapeleke watoto kupata chanjo hiyo. Malengo yetu ni kuwapa chanjo watoto wote.

8. Lishe bora ni muhimu kwa familia. Kula samaki mboga mayai, wanga na nyama kadiri inavyowezekana.
9. Nawashukuru kwa jinsi mnavyoniunga mkono, nami nawapenda sana.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages