Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga (wa pili kushoto) akiwasili katika Hotel ya White Sands jijini Dar es Salaam kujionea jinsi Hoteli hiyo iliyopo ufukweni mwa bahari inavyotunza mazingira yake. Kulia ni Meneja Mkuu wa Hoteli ya White Sands Alwyn Kellerman na Afisa Mazingira wa Hoteli hiyo Bi. Linda Mbuya.
Mmoja wa wafanyakazi wa Hoteli hiyo akifunua chemba inayopitisha maji taka kwa ajili ya kukaguliwa na jopo la wataalam kutoka NEMC na Maafisa wa Wizara. Katika ukaguzi huo Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga hakuridhishwa na jinsi hoteli hiyo inavyoendesha mfumo wake wa maji taka na kuagiza timu ya wataalam kutoka NEMC kufanya ukaguzi upya wa mifumo hiyo.
Meneja Mkuu wa Hoteli ya Giraffe Ocean View Bw. Nicholas Oyieko akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Mh. Kitwanga (wa pili kushoto) jinsi hoteli hiyo inavyotunza mazingira na namna inavyodhibit mfumo wake wa maji taka kuhakikisha kwamba haileti madhara.
Hii ni sehemu iliyoko pembeni ya Hoteli ya Giraffe ambayo mmiliki wake hafahamiki ambayo imewekwa uzio na kufanya bahari kushindwa kupumua vizuri na kusababisha mkusanyiko wa uchafu unaodaiwa kutuama mahali hapo tangu mafuriko ya hivi karibuni yaliyoikumba jiji la Dar es Salaam. Naibu Waziri ameamuru muhusika kutafutwa mara moja na kupigwa faini na kuamuriwa kuondoa vifusi hivyo.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga na ujumbe wake wakiangalia eneo hilo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)