NA: GLADNESS MUSHI -ARUSHA
MKUU
wa Mkoa wa Arusha amemzawadia tuzo ya uandishi bora wa habari za
jamii na maendeleo Meru , mwandishi wa habari Mary Mwita wa magazeti
ya Mtanzania na Rai ya Kampuni ya New habari (2006) LTD.
Mkuu wa Mkoa huyo ametoa tuzo
hiyo ,ikiwa ni ahadi yake ,na agizo alilotoa kwa uongozi wa Halmashauri
hiyo kupeleka jina la Mwandishi wa habari aliyeandika habari bila
kupotosha jamii katika Halmashauri hiyo ,na kuweza kumpata Mwandishi
huyo .
Mkuu alitoa Tshs 500,000 ikiwa ni
tuzo na kiasi cha fedha zilizokabidhiwa kwa wadau wengine mwaka huu
waliobainika kuchangia maendeleo ya Meru.
Mkuu huyo alisema kuwa huwezi
kutaja maendeleo bila kuhusisha vyombo vya habari na waandishi wa habari
,na kuwa kila Halmashauri inatakiwa kutambua mchango wa maendeleo ya
wadau ikiwa ni pamoja na waandishi wa habari .
Akimpongeza Mwandishi Mary Mwita
,alisema wakati umefika wa waandishi wa habari kuandika habari za
kweli bila kupotosha umma ,ikiwa ni kuwawezesha wananchi kujifunza na
kupata ujuzi kupitia habari hiyo ,badala ya kuandika habari za uongo .
Mlongo alisema kuwa ni wazi kuwa
kila mtu katika jamii akisimama katika nafsi yake kulingana na karama
aliyopewa Maendeleo ya haraka yatafikiwa na kuwawezesha wananchi
kupunguza kasi ya umaskini katika jamii .
Katika hatua nyingine alipongeza
uongozi wa Halmashauri ya Meru kwa kutambua mchango wa maendeleo ya
wadau na kutaka Halmashauri nyingine kuiga mfano huo wa kutunikia
zawadi wadau waliosaidia maendeleo ya Halmashauri.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Meru Trisas Kagenzi alisema kuwa zoezi la
kuwazawadia wadau ni endelevu ,na kuwa wataendelea kutambua mchango wao
kwa kuwa bila ushirikiano na wadau wa maendeleo ,maendeleo yanaweza
kuchelewa .
Kagenzi alisema kuwa Mwandishi
Mary Mwita ,amekuwa akiandika habari bila kupotosha umma kwa kujituma
na kutaka waandishi wengine kuiga mfano wake.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)