Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon akifafanua jambo wakati wa mkutano wake wa mwisho wa mwaka na Klabu ya Waadishi wa Habari wa Umoja wa Mataifa ( hawapo pichani). Katika Mkutano huo ambao ulifanyika siku ya jumatano aliutumia kuelezea mafanikio na changamo za utendaji kazi wa UM katika mwaka unaomalizika. Pia alielezea jitihada anazozifanya katika kuutafutia ufumbuzi mgogoro wa eneo la Mashiriki ya DRC. Akabainisha kwamba katika siku tano zilizopita amekuwa akifanya mazungumzo kwa njia ya simu na baadhi ya viongozi wa Afrika kwa lengo la kupata mchango na maoni yao kuhusu mpango mpana wa kisiasa anaojaribu kuuanda kwajili ya DRC hususani eneo la Mashiriki. Miongoni mwa Marais ambao Ban Ki Moon amefanya nao mazungumzo ni Rais wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.
-
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)