Katibu
Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (kulia) akijadiliana jambo kuhusiana
na mkutano mkubwa wa kimataifa wa ushirikiano kwa manufaa ya wote, Smart
Partnership Dialogue ‘Global 2013’, unaotarajiwa kufanyika hapa nchini
mwezi Mei mwaka 2013 alipokua akiongea na wanahabari jijini la Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki, (katikati) ni Kaimu katibu Mtendaji wa Baraza
la Taifa la Biashara (TNBC), Bw. Samson Chemponda na kushoto ni Meneja
Mradi wa Smart Partnership Dialogue ‘Global 2013,’ Rosemary Jairo.
Katibu
Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (kulia) akijadiliana jambo kuhusiana
na mkutano mkubwa wa kimataifa wa ushirikiano kwa manufaa ya wote, Smart
Partnership Dialogue ‘Global 2013’, unaotarajiwa kufanyika hapa nchini
mwezi Mei mwaka 2013 alipokua akiongea na wanahabari jijini la Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki, (katikati) ni Kaimu katibu Mtendaji wa Baraza
la Taifa la Biashara (TNBC), Bw. Samson Chemponda na kushoto ni Meneja
Mradi wa Smart Partnership Dialogue ‘Global 2013,’ Rosemary Jairo.
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Viongozi
katika ngazi mbalimbali Tanzania wamepewa changamoto kutoa umuhimu
mkubwa na kushiriki kikamilifu katika majadiliano ya ushirikiano kwa
manufaa ya wote (Smart Partnership Dialogue) ili kuchochea haraka
maendeleo katika nchi.
Wito huu
umetolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alipokua akiongea
na waandishi wa habari kuhusiana na matayarisho ya mikutano ya kitaifa
na ule wa kimataifa kuhusiana na majadiliano hayo hapa nchini.
“Ningewataka
viongozi nao watoe umuhimu mkubwa kwenye jambo hili kwa sababu
watanufaika sana kupata mawazo mbalimbali ya wananchi,” alisema Balozi
Sefue mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa viongozi
washiriki katika majadiliano katika ngazi zote kitaifa na pia wajiandae
na majadiliano ya kimataifa.
Haya ni majadiliano yanayolenga kutoa fursa kwa jamii kukaa pamoja na kuzungumzia maswala mbalimbali ya maendeleo.
Kwa hapa
Tanzania, chombo kitakachosimamia na kuratibu majadiliano haya kitaifa
ni Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) wakati Wizara ya Mambo ya Nje ina
jukumu la kuratibu mkutano wa kimataifa kuhusu majadiliano hayo hapa
nchini mwezi Mei, 2013.
Mchakato wa majadiliano haya ulishazinduliwa na Rais Jakaya Kikwete tangu Mei, 2012.
Balozi
Sefue ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya TNBC alisema
kwamba kila mtanzania ajitahidi kuelewa dhana hii kwa kusoma na
kusikiliza vyombo vya habari kwa sababu ni fursa nzuri kwa kila
mwananchi kushiriki katika maendeleo ya nchi na namna tunavyoweza
kufikia maendeleo ya haraka.
“Hakuna
mwenye ukiritimba wa mawazo kwa hiyo tunahitaji mawazo ya kila mwananchi
na hivyo kila mtu ajione kuwa ana wajibu wa kuchangia maana faida
itakua kwa kila mmoja na nchi kwa ujumla,” alisema.
Alisema
dhana hii ya majadiliano kwa manufaa ya wote ni muhimu sana hasa kwa
viongozi kwa kuwa kadiri kiongozi anavyopata maoni ya watu wengi zaidi,
ndio maamuzi yake yatakavyokua sahihi zaidi na yatazingatia mahitaji ya
makundi mbalimbali katika jamii.
“Kwa
mfano, maamuzi ya serikali yatakubalika kwa urahisi zaidi na wananchi
kwa sababu watakua wameshiriki katika kuyaandaa,” alisema.
Akielezea
zaidi alisema kujenga nchi kunahitaji makundi yote kwa hiyo ni vyema
watu wakipata fursa nyingine kukakaa pamoja na kujadili mambo ya msingi
ya maendeleo.
Alisema
majadiliano kama haya ni fursa nyingine ya kushirikisha wananchi na
wadau wengine katika kuhakikisha kuwa mipango katika kutekeleza Mpango
wa Taifa wa Miaka Mitano na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 inazingatia
maoni na inakua na faida kwa kila kundi katika jamii.
Mkutano
wa mwezi Mei, 2013 ni mwendelezo wa mikutano kama hii ambayo imeanza
kiasi cha miaka kumi na tano iliyopita na ikianzishwa na Jumuia ya
Madola kupitia taasisi yake inayoitwa Commonwealth Partnership for
Technology Management na kwa ushiriki mkubwa wa aliyekuwa waziri Mkuu wa
Malaysia, Dkt. Mahathir Mohammed.
Tayari
TNBC imeshaanza kuendesha semina za uhamasishaji zenye lengo la kutoa
ufahamu kuhusu majadliliano ya kitaifa kabla ya yale ya kimataifa.
Kitaifa,
majadiliano haya yatahusisha makundi mbalimbali yakihusisha serikali,
wanasiasa, wafanyabiashara, wasomi,wafanyakazi, vijana, wasanii na
wakulima ambao watakaa pamoja na kujadili maswala mbalimbali yanayohusu
biashara na maendeleo.
Makundi
haya yatapata fursa hiyo kupitia mabaraza ya mikoa na yale ya wilaya ya
TNBC ambako madajiliano hayo yatafanyika kuanzia huko hadi ngazi za
kitaifa kabla ya majadiliano ya kimataifa mwezi Mei.
Makundi yote yatapata fursa ya kujadili na kutoa mapendekezo yao.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)