Pages

YAFAHAMU MAPOROMOKO YA MAJI YA MTO KALAMBO MKOANI RUKWA YA PILI KWA UKUBWA BARANI AFRIKA

 
Kalambo Falls ambayo ni maporomoko makubwa ya maji ya asili yanayochukua nafasi ya pili kwa ukubwa barani Africa yakiwa na urefu wa mita 235 yanapatikana Mkoani Rukwa mpakani na nchi jirani ya Zambia ni miongoni mwa vivutio vya asili nchini Tanzania vyenye hadhi ya kupigiwa kura kuwa miongoni mwa maajabu saba ya asili nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla. Vivutio vya Tanzania vinavyoshindanishwa na vingine tisa (9) barani Afrika katika nafasi ya maajabu saba barani Afrika ni Mlima Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro na hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Pigia vivutio hivi vitatu na vingine vinne ikiwemo Kalambo Falls kupata vivutio 7 vya maajabu ya asili nchini Tanzania na barani Afrika.
PIGA KURA YAKO KUPITIA HAPA http://sevennaturalwonders.org/tanzania

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya alipotembelea maporomoko hayo hivi karibuni.
Mbunge Viti Maalum CCM Geita Vicky Kamata alipotembelea maporomoko hayo hivi karibuni kwa ajili ya kupiga picha za kutangaza kivutio hicho na vinginevyo vinavyopatikana katika Mikoa ya Rukwa, Katavi na Tanzania kwa ujumla.
Kalambo Falls.(Picha na Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)