Uongozi
wa Jumuiya ya Watanzania New York na Vitongoji vyake, NYTC (Board na
Executive Committee), wanafurahi kuwaalika Watanzania wote wanaoishi New
York na Vitongoji vyake, kwenye sherehe ya kuwakaribisha Balozi Manongi
na Naibu wake Ndugu Mwinyi, viongozi wapya wa Uwakilishi wa Kudumu wa
Tanzania katika Umoja wa Mataifa New York, pia kumshukuru Dr. Seruhere
aliyekuwa Naibu Balozi wa muda na Mlezi wa NYTC.
Sherehe hii itafanyika Jumamosi, tarehe 1 December kuanzia saa 12 jioni
mpaka saa 6 usiku kwenye ukumbi wa:
Holy Trinity Greek Orthodox Church
10 Mill Road
New Rochelle, NY 10804
Wote mnakaribishwa.
Tunaomba mchango wa dola 25 kutoka kwa kila mtu, na wanafunzi dola 10
kwa ajili ya gharama ya shughuli nzima. Huu mchango upelekwe kwa
wafuatao kabla ya terehe 20 November 2012, Receipts za mchango
zitatolewa .
Miriam Abu (914) 316-2814
Amir Kius (201) 450-5129
Catherine Kyauka (201) 562-2890
Shabani Mseba (347( 712-8539
Tunatanguliza shukrani zetu za dhati.
Uongozi wa NYTC.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)