Pages

UHABA WA MADARASA WAENDELEA KUITESA SHULE YA MSINGI RWENGERA DARAJANI

 Nyumba ya mwalimu inapotumika kama darasa.Kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa Shule ya Msingi Rwengera Darajani Wilaya ya Korogwe imeamua kutumia nyumba hii ya mwalimu kama darasa la awali kwa muda.
 Hili ni moja ya darasa la Shule ya Msingi Kitopeni Wilaya ya Korogwe, kutokana na Bajeti ya Wizara husika kuwa finyu limeshindwa kufanyiwa marekebisho na kutumiwa vivyo hivyo, darasa hili halina sakafu wala madawati ya kutosha wanafunzi hukaa chini kwenye vumbi. Mwalimu aingiapo darasa hutamani wanafunzi wasiinuke kumsalimu maana vumbi linavyotimka wainukapo ni hatari.
 Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Msandaka, Manase Kijo akionesha moja ya kitabu cha somo la Tenolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) anasema somo hili ni changamoto kwa baadhi ya shule kwani hulazimika kufundishwa na walimu ambao hawana ujuzi wa somo hilo huku kukiwa hakuna vifaa husika (kompyuta).
 Hapa si kwamba walimu wameamua kupumzika nje kukimbia joto ofisini ‘No’ Shule hii ya Msingi Silabu yenye darasa la kwanza hadi la saba haina ofisi ya walimu hivyo chini ya mti huu wameamua kufanya ofisi ya walimu na pia ofisi ya Mkuu wa Shule. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Mizeki Charahani akiwa na mwalimu Julias Mokiwa wa shule hiyo. Hata hivyo kwa sasa kunaujenzi unaendelea ili kuweka mambo sawa hapo mbeleni.
Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Msandaka, Manase Kijo akionesha moja ya changamoto ambazo hukumbana nazo walimu kutokana na mabadiliko ya mara kwa mara ya vitabu vya masomo bila maandalizi fasaha, shule hiyo ipo katika Manispaa ya Moshi Mkoa wa Kilimanjaro.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)