TIMU YA NMB FC YAKUBALI KICHAPO CHA MAGOLI 2 KWA 1 DHIDI YA EXIM FC - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TIMU YA NMB FC YAKUBALI KICHAPO CHA MAGOLI 2 KWA 1 DHIDI YA EXIM FC


Mshambuliaji wa Exim FC, Erick Makule (kushoto) na mchezaji wa NMB F.C Omar Said (kulia) wakipigania mpira, katika mechi ya kirafiki iliyofanyika uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam jumapili jioni. Mechi ilimalizika kwa Exim F.C kuifunga NMB F.C 2-1. 
Mshambuliaji wa Exim FC, Ammy Ditufu (kulia) na mchezaji wa NMB F.C (kushoto) wakipigania mpira, katika mechi ya kirafiki iliyofanyika uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam Jumapili jioni. Mechi ilimalizika kwa Exim F.C kuifunga NMB F.C 2-1.
Na Mwandishi Wetu. 


TIMU ya mpira wa miguu ya benki ya Exim ya Tanzania, Exim F.C imeendeleza wimbi la ushindi katika michezo yake ya kirafiki, baada ya kuifunga timu ya NMB  magoli 2-1. 

Mchezo huo uliochezwa jana katika uwanja wa Karume ulianza kwa kasi hasa kutokana na timu hizo kuwa na upinzani mkubwa pale zinazopokutana.

Jambo hilo lilisababisha timu zote kuanza mchezo kwa kasi huku Exim ikionekana kuwa imara zaidi hasa kutokana na kusheheni wachezaji imara waliokuwa wanapeleka mashambulizi mara kwa mara langoni mwa NMB.

Dakika ya 5, NMB iliweza kupata goli la kwanza baada ya faulo iliyopigwa  na Aron Nyanda na kumkuta Nuhu Mkuchu.

Kuingia kwa goli hilo kuliamsha mashambulizi kwa timu ya Exim, ambayo ilifanya mabadiliko kwa kumtoa Richard Noni na kumuingiza Ami Ditufu.

Mabadiliko hayo yalionekana kuisaidia zaidi Exim, baada ya kuanza kulishambulia lango la NMB kama nyuki na kupelekea kukosa magoli ya wazi katika dakika ya 15, 17 na 20 kupitia kwa wachezaji wake Fadhili Selemani na Norbert Missana.

Kipindi cha pili kilipoanza, NMB walionekana kuzidiwa huku Exim ikindandaza kandanda safi na kuwasaidia kusawazisha goli kupitia kwa Ditufu.

Ditufu alishinda goli hilo, baada ya kupokea pasi safi ya  Missana na yeye kupiga shuti lililozaa goli hilo la kwanza kwa Exim.

Kuingia kwa goli hilo, kuliamsha ari ya ushindi kwa Exim  ambao walicheza vyema na kufanikiwa kufunga goli la pili kupitia kwa Missana.

Missana alishinda goli hilo katika dakika ya 57 na kuwafanya NMB kuzidi kupoteana na kuipa nafasi zaidi Exim kutawala mchezo huo. 

Hadi filimbi ya mwisho Exim ilifanikiwa kutoka uwanjani na ushindi huo wa magoli 2-1.

Akizungumza baada ya mchezo huo, nahodha wa Exim Fadhili Selemani alisema wanafurahi kuifunga NMB ambao ni wapinzani wao wakubwa.

“Hawa ni wapinzani wetu hivyo kuwafunga ni mwanzo tu, kwani tumejiandaa kuwafunga kila mechi hasa kutokana na kuwahi kutufunga michezo miwili”alisema.

Hivyo, alisema ushindi huo ni mwanzo kwa kuwa kila siku wanafanya mazoezi ya nguvu ili kuhakikisha wanashinda michezo yao yote.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages