Mstahiki Meya akifungua Tamasha.
Mama Balozi akiwaonyesha wageni Rasmi Mameya vitu mbalimbali vitakavyouzwa kwa ajili ya kuchangia mfuko huu.
Mtahiki Meya akiangalia sehemu ya chakula ya Tanzania.
kutoka Kushoto Mh balozi wa Grenada Ruth Elizabeth Rouse, Mtahiki Meya Christopher Buckmaster na Mama Balozi Joyce Kallaghe.
Mama Kiondo akiwa kikazi zaidi kuitangaza Tanzania Pics .
Mama Balozi Akipakwa Hina kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa elimu
Mama Balozi akimkabidhi Mayorese Mrs. Anne Hobson baada ya kununua kitenge katika banda la Tanzania .
Mayorese Mrs. Anne Hobson katika banda la Tanzania.
wateja wakinunua bidhaa kutoka banda la Tanzania.
Sherehe ikiendeleaPics By Frank Eyembe.
Ukumbi wa Royal Borough of Kensington.Pics By Frank Eyembe.
---
Salaam,
Jumuiya
ya Commonwealth Countries League (CCL) inayoshirikisha nchi hamsini na
nne (54) duniani kutoka katika jumuiya ya madola iliandaa tamasha maalum
siku ya jumamosi tarehe 3.11.12 kwa ajili ya kuchangia mfuko wa
kumsaidia na kumwezesha msichana kusoma elimu ya sekondari.
Historia ya
Commonwealth Countries League ilianzishwa rasmi kutoka kwa baadhi ya
wanawake mnamo mwaka 1923 nchini Australia kwa ajili ya kusaidia
kutangaza uelewa wa haki sawa kati ya wanawake na wanaume waliopo nchi
mbalimbali zilizo ndani katika jamuiya ya madola.
Tamasha hili
lilifanyika Royal Borough of Kensington chini ya uongozi kutoka kwa
Mh. Balozi wa Grenada Ruth Elizabeth Rouse ambaye ndio raisi wa jumuiya
hiyo akisaidia na makamu wake mama Balozi Joyce Kallaghe. Wageni Rasmi
walikua Wastahiki Mameya wa Worshipful Royal Borough of Kensington na
Chelsea - Councillor Christopher Buckmaster na Mrs. Anne Hobson Shughuli ya mwaka huu iliandaliwa na wake za
mabalozi kutoka katika jumuiya za Madola hamsini na nne (54) ili
kuchangisha pesa kwa njia ya kuuza vitu mbalimbali vya asili kama
chakula, urembo, maua, vinywaji n.k. Fedha zote zilizopatikana
zilipelekwa kusaidia mfuko huu wa Elimu kwa ajili ya kumsomesha mtoto wa
kike.
Aidha Mama
Balozi Joyce Kallaghe aliongeza kwa kusema ''Elimu ni Ufunguo Wa Maisha
kumsomesha mwanamke ni kuiwezesha jamii nzima hivyo vipaumbele vyote
vimeelekezwa kwa kwa ajili ya kuwasomesha watoto wa kike walio maskini
au wanaoishi katika mazingira magumu ambao wana uwezo wa kuendelea
kusoma elimu ya sekondari katika nchi za jumuiya ya Madola". Tangu
mwaka 2011/2012 mfuko wa Elimu wa CCL ushawawezesha watoto wa kike 364
kutoka nchi 25 ikiwapo Tanzania. Pia aliwasihi wadau kuwa wazalendo kwa
kuchangia mfuko huu kwa kuwasiliana kupitia barua pepe ccl.edfund@googlemail.com
Kiasi cha paundi mia moja hamsini (£150) na Mia nne na hamsini (£450) zinatosha kumsomesha msichana kwa mwaka mzima
Asanteni
Urban Pulse Creative
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)