Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada (katikati) pamoja na
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya TALIA ya mjini Mtwara, Ayubu Samuel wakitiliana saini mkataba wa makubaliano kati ya
ubalozi wa japan na TALIA kwaajili ya ujenzi wa mradi wa upanuzi wa shule ya wenye ulemavu Dinyecha
Wilayani Mtwara utakao gharimu zaidi ya shilingi Milioni 192 na ujenzi.
Anaeshuhudia kulia ni Waziri wa TAMISEMI, Hawa Ghasia.
Mkurugenzi wa taasisi Women in Social Entrepreneurship
(WISE) ya mkoani Lindi, Astronaut Bagile (kushoto) akitiliana saini na Balozi
wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada (wa
tatu kulia) msaada wa ujenzi wa
bweni la wasichana sekondari ya Ngapa ya Lindi utakaogharimu shilingi Milioni
188. Wengine wanaoshuhudia utiaji saini huo kutoka kushoto ni Meya wa
Manispaa ya Lindi, Frank Maghali, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila, Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Nassor Hamid
Nassor na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi, Ashimun Mnzava.Utiaji saini huo wa makubaliano
hayo ya msaada ulifanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi Novemba 7, 2012.
Waziri wa TAMISEMI, Hawa Ghasia, akizungumza jambo wakati wa utiliaji saini huo
uliofanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Novemba 7, 2012. Kushoto ni Balozi
wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada
Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki
Okada akisoma hotuba yake kwa viongozi wa mkoa wa Lindi na Taasisi ya Women in Social
Entrepreneurship (WISE) ya mkoani Lindi wakati wa utilianaji saini mkataba wa
makubaliano kati ya Ubalozi wa Japan na Taasisi ya WISE msaada wa ujenzi wa
bweni la wasichana sekondari ya Ngapa ya Lindi utakaogharimu shilingi Milioni
188. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila na kulia ni
Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Nassor Hamid
Nassor.
Balozi wa Japan akiwa katika picha ya
pamoja na viongozi wa Mkoa wa Lindi na viongozi wa taasisi ya WISE baada ya
kutiliana saini. Kutoka kushoto mstari wa mbele ni Meya wa Lindi, Frank Maghali, Balozi
wa Japan, Masaki Okada , Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick
Mwananzila, DC wa Lindi, Nassor Hamid Nassor na Makurugenzi Mtendaji wa WISE, Astronaut
Bagile.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)