Kampuni
ya MultiChoice imetangaza punguzo la asilimia 10 ya malipo ya mwezi kwa
wateja wa televisheni kwa vipindi vya DStv litakaloanza kesho Novemba
15, 2012.
Meneja Mkuu waMultiChoice
Tanzania, Peter Fauel alisema punguzo hilo litawawezesha wateja wao
kulipia huduma za matangazo ya televisheni ya kituo hicho kwa gaharama
nafuu.
Fauel alisema kwa wateja
watakaokuwa wamelipia tayari huduma hiyo ndani ya mwezi huu, wataendelea
kutumia hadi pale mwezi utakapokuwa umeisha, kisha wataanza na bei mpya
ya punguzo kuanzia mwezi unaofuata ila wahakikishe huduma yao
kutokatika.
“Tumedhamiria kuwapunguzia wateja wetu gharama kubwa kulingana na hali halisi ya maisha ya mwananchi wa kawaida,” alisema Fauel. Meneja mkuu huyo alisema, kuwa
kama kawaida yao huwapa wateja wao unafuu wa bei kulingana na kipato
chao, hivyo punguzo hilo litawanufaisha kwa kiwango kikubwa ili kila
mmoja afaidi burudani.
Alisisitiza kuwa DStv itaendelea
kuwapatia Watanzania na Waafrika kwa ujumla vipindi vyenye ubora kwa
vile wamewekeza katika vipindi vipya. Kwa wateja watakaonufaika na ofa hii, wataweza kupunguza gharama za kulipia huduma yao ya DStv kwa 150,000 kwa mwaka!
Fauel akaongeza kwamba “Tunawaahidi wateja wetu huduma bora
na kwamba kwetu mteja ni mfalme. Mtandao wetu wa usambazaji unazidi
kupanuka na sasa tupo kila mkoa wa nchi. Pia tunafurahi kwamba sasa tuna
ofisi zetu Kariakoo na supermarket ya Uchumi iliyopo barabara ya Pugu.
Hii itawarahisishia wateja wetu kupata bidhaa na huduma zetu kwa haraka
zaidi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)