Bondia
maarufu kuliko wote Tanzania Francis Cheka atamvaa Udiadia Mwahia
kutoka nchini DRC Kongo kugombea mkanda wa ubingwa wa IBF katika bara la
Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi.
Mabondia hao watakutana katika mpambano wa kwanza tangu Arusha liwe jiji katika uwanja wa Shekh Amri Abeid tarehe 26 Desemba 2012 siku ya Boxing Day!
Akimtambulisha Francis Cheka kwa waandishi wa habari katika ukumbi wa Melezo jijini Dar-Es-Salaam leo, mratibu wa mpambano huo na ambaye alishawahi kuwa bingwa wa Tanzania kwenye ngumi za ridhaa George Andrew alisema kuwa bondia Udiadia Mwahila anakaa Lusaka Zambia ambako ndipo anapofanya shughuli zake za ngumi chini ya promota maarufu Anthony Mwamba!
Udiadia ana rekodi ya mapambano 12 na ametoka sare pambano
moja na hajapoteza hata moja wakati Francis Cheka ana rekodi ya
mapambano 33 amepoteza 6 na kutoka sare pambano moja.
Geporge alisema kuwa mpambano huo utatumika kulitangaza jiji la Arusha kama Las Vegas ya ngumi katika bara la Afrika na kulifananisha jiji la Arusha na jiji la Geneva lililoko nchini Switzerland.
Mpambano huo unakuja wakati ambapo mpambano mwingine wa Francis Cheka na bondia kutoka Ujerumani wa kugombea mkanda wa IBF wa mabara ulifutwa baada ya Simon kuumia katika mazoezi.
Naye Rais wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati,
Ghuba ya Uarabu na Ghuba ya Uajemi Onesmo Nhowi alisema kuwa wao kama
IBF wamesharuhusu maandalizi ya mpambano huo. Rais huyo aliwataka
wadhamini pamoja na wananchi wa mkoa wa Arusha na mikoa mingine
kujitokeza kwa wingi ili kulifanya pambano hilo kuwa la mafanikio.
Naye bondia Francis Cheka alisema kuwa amejiandaa kwa kiasi
kikubwa na atazidi kufanya mazoezi ili kupata ushindi kwake pamoja na
nchi ya Tanzania. Aliendelea kusema kuwa kila Mtanzania anajua uwezo
wake kwa hiyo amewataka wote wafike kwa wingi ili kupata uhondo na
burudani tosha
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)