...................................................
Nimesafiri
na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe mkuu wa mkoa wa Katavi
nikienda huko kwa mwaliko wa mkuu wa mkoa huyo kwa ajili ya shughuli maalum
ya kumuvuzisha matukio katika uzinduzi rasmi wa mkoa huo utakaofanyika
Novemba 25 mwaka huu mjini Mpanda ukizinduliwa na Makamu wa Rais Dkt.
Gharib Bilal.
Lakini tukiwa njiani
tumepitia kwenye shamba la Mh. Dkt. Rajab Rutengwe lililoko huko
Bagamoyo Mkoani Pwani katika kijiji cha Mboga mbele kidogo ya kijiji cha
Msoga nyumbani kwa Mh Rais Jakaya Kikwete, Mh. Dkt. Rutengwe pamoja na
majukumu yake ya uongozi katika mkoa wa katavi ni mkulima mzuri kwa
shamba lake lina ukubwa wa hekari 15 na amepanda mazao mbalimbali
yakiwemo Maembe, Mananasi, Mapapai Michungwa na pia anaendesha ufuganji
wa nyuki na kuku jambo ambalo limekuwa mfano kwa wakazi wa kijiji hicho.
Mh.
Dkt. Rutengwe anasema kwa kweli hawezi kununua kiwanja ambacho hakina
eneo la kilimo kwani ukulima kwake ni jambo muhimu sana na ndiyo maana
aliamua kuanzisha kilimo cha kisasa katika kijiji hicho kwa kupanda
mazao mbalimbali kitu ambacho kimenifanya kuwa mkulima wa mfano katika
kijiji chetu.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)