Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu
---
Sehemu ya 11 ya Kanuni ya Bunge, Ibara ya 121 inaeleza kuwa
mbunge yeyote anaweza kuwasilisha kwa Spika taarifa ya hoja ya kumshtaki
Rais kwa madhumuni ya kumuondoa Rais madarakani kupitia azimio la Bunge
kwa mujibu wa Ibara ya 46 A ya Katiba ikiwa inadaiwa kwamba Rais;
ametenda vitendo ambavyo kwa ujumla vinavunja katiba au sheria ya
maadili ya viongozi wa umma.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Bunge jana, Lissu alisema amechukua uamuzi huo baada ya kuona Bunge limeikalia ripoti ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge iliyomhoji kuhusu kauli yake ya kuwatuhumu majaji kuwa baadhi yao hawana sifa.
SIKU moja baada ya Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu
Lissu kusema atawasilisha hoja ya kumshtaki Rais Jakaya Kikwete iwapo
atashindwa kuwaondoa kazini majaji wasio na sifa aliowateua, Ikulu
imemwambia aendelee na mchakato wake.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu
alisema jana kuwa hakuna anayemzuia Lissu kushtaki kama anaona kuna
sababu za kufanya hivyo.“Lissu ni Mbunge na ana haki zake za msingi na
kama amefikia hatua hiyo anaweza kufanya hivyo... hakuna mtu ambaye
anaweza kumkataza. Nani mwenye uwezo wa kuingilia uhuru wa mtu?”
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Bunge jana, Lissu alisema amechukua uamuzi huo baada ya kuona Bunge limeikalia ripoti ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge iliyomhoji kuhusu kauli yake ya kuwatuhumu majaji kuwa baadhi yao hawana sifa.
Alisema ameamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuona Rais Kikwete ambaye
ana mamlaka ya kuteua majaji, ameshindwa kuwaondoa kazini majaji hao
wasiokuwa na sifa.Kwa habari zaidi bofya na Endelea...>>>>>>
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)