Pages

Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu,Salva Rweyemamu:''Hatuwezi kumzuia Mheshimiwa Mbunge Tundu Lissu kumshtaki Rais Jakaya Kikwete''.

Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu 
--- 
Sehemu ya 11 ya Kanuni ya Bunge, Ibara ya 121 inaeleza kuwa mbunge yeyote anaweza kuwasilisha kwa Spika taarifa ya hoja ya kumshtaki Rais kwa madhumuni ya kumuondoa Rais madarakani kupitia azimio la Bunge kwa mujibu wa Ibara  ya 46 A ya Katiba ikiwa inadaiwa kwamba Rais; ametenda vitendo ambavyo kwa ujumla vinavunja katiba au sheria ya maadili ya viongozi wa umma.
 SIKU moja baada ya Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu kusema atawasilisha hoja ya kumshtaki Rais Jakaya Kikwete iwapo atashindwa kuwaondoa kazini majaji wasio na sifa aliowateua, Ikulu imemwambia aendelee na mchakato wake.

Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu alisema jana kuwa hakuna anayemzuia Lissu kushtaki kama anaona kuna sababu za kufanya hivyo.“Lissu ni Mbunge na ana haki zake za msingi na kama amefikia hatua hiyo anaweza kufanya hivyo... hakuna mtu ambaye anaweza kumkataza. Nani mwenye uwezo wa kuingilia uhuru wa mtu?”

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Bunge jana, Lissu alisema amechukua uamuzi huo baada ya kuona Bunge limeikalia ripoti ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge iliyomhoji kuhusu kauli yake ya kuwatuhumu majaji kuwa baadhi yao hawana sifa.
 
 Alisema ameamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuona Rais Kikwete ambaye ana mamlaka ya kuteua majaji, ameshindwa kuwaondoa kazini majaji hao wasiokuwa na sifa.Kwa habari zaidi bofya na Endelea...>>>>>>

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)