MDAU MANYERERE AWAJIBU MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MDAU MANYERERE AWAJIBU MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

Hapo Chini Ni Taarifa Kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania

 HAPA CHINI NI MDAU MANYERERE ALIVYOWAJIBU MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
 
Wakati mwingine Mamlaka ya Hali ya Hewa inawapa sifa za bure baadhi ya watu kutokana na kushindwa kwake kuwa na utabiri wa kisayansi. Itakumbukwa kuwa Mamlaka iliposema kutakuwapo mvua za El Nino, Mzee wa Upako; akatangaza kwa kuapa kabisa kwamba endapo mvua hizo zingenyesha, basi angeacha kuhubiri! Kweli, mvua hizo zimepotea, na sasa Mamlaka inathibitisha kuwa hazipo!!

Hatari ninayoiona hapa ni kwamba wananchi watakuwa na imani zaidi na wachungaji (hata kama wamo waongo) kuliko Mamlaka inayoendeshwa na wanasayansi! Pengine ni muhimu basi, Mamlaka kutofuja fedha kwa kwenda Nairobi kwenye mkutano ulioandaliwa, badala yake wamfuate Mzee wa Upako ili awaeze hiyo hali ya "hewa isiyokuwa ya kawaida" maana yake ni nini, na itakuwa na athari gani? Nashauri hiyo kwa sababu inaelekea maono yake ni zaidi ya utabiri wa wanasayansi wetu.

Haitashangaza kuona Kanisa la Mzee wa Upako likijaa hadi pomoni kutokana na "utabiri" wake huu ambao umekuwa wa kweli kuliko wa Mamlaka ya Hali ya Hewa.

Nawasilisha.

Manyerere

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages