MALAWI YARUHUSU NDOA ZA JINSIA MOJA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

MALAWI YARUHUSU NDOA ZA JINSIA MOJA


Rais Banda wa Malawi: Ushoga Ruksa!
SHERIA ya kukataza ndoa za jinsia moja nchini Malawi imesitishwa kwa muda mpaka hapo uamuzi utakapotolewa na Serikali.

Serikali ililiagiza jeshi la polisi kutowakamata watu wanaojihusisha na ndoa za jinsia moja , mpaka hapo uamuzi utakapotolewa rasmi na Serikali.

Awali Mapenzi ya jinsia moja nchini Malawi yalipigwa marufuku na kutolewa kifungo cha miaka hadi kumi na minne jela kwa wanaokamatwa kushiriki.

Baadhi ya viongozi wa kimagharibi walitishia kusitisha kuzipa msaada nchi za Afrika ambazo zinakataa kutambua haki za mashoga

Ushoga ni haramu katika nchi nyingi za Afrika na linasalia kuwa swala tete katika jamii nyingi za Afrika zenye kukumbatia maadili ya kiafrika.

Mmoja wa viongozi wa kijamii wenye ushawishi mkubwa, Kaomba, aliiomba serikali kutoruhusu bunge kubadili sheria zake kuhusu ushoga. ''Hii ni kinyume na maadili'' alisema kiongozi huyo.

Mnamo mwaka 2010, wanaume wawili walikamatwa na kushtakiwa kwa utovu wa nidhamu hadharani baada ya kusema kuwa wataoana.

Kesi hiyo ilivutia sana kero kutoka kwa jamii ya kimataifa na hata kusababisha baadhi ya wahisani kusitisha msaada kwa nchi hiyo, na ikawa pigo kubwa kwa nchi hiyo ambayo ni moja ya nchi maskini zaidi duniani.

Rais wakati huo akiwa , Bingu wa Mutharika - aliwasamehe wanaume hao kwa misingi ya kibininadamu ingawa alisisitiza kuwa ni kinyume na maadili ,na tamaduni za kiafrika na hata sheria za nchi.

Hata hivyo Rais Joyce Banda, aliyemrithi Bingu aliwaambia wabunge kuwa anataka kubatilisha sheria hiyo na kuhalalisha mapenzi ya jinsia moja.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages