Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simu za Mkononi, Sam Elangalloor,
wakifunua kitambaa kwa pamoja kuashiria uzinduzi wa Shule ya Msingi
Kiromo, iliyopo Wilaya ya Bagamoyo-Mkoa wa Pwani, iliyokarabatiwa na
Kampuni ya Airtel Tanzania. Uzinduzi huo umefanyika leo.
wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisikiliza maelezo kutoka kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Dkt. Shukuru Kawambwa (kulia) wakati akionyeshwa madawati yaliyotolewa
na Kampuni hiyo simu za mkononi ya Airtel Tanzania, kwa Shule ya Msingi
Kiromo, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Shule hiyo baada ya kukamilika
kwa ukarabati, iliyofanyika shuleni hapo leo. Wa tano (kushoto)
ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simu za Mkononi, Sam Elangalloor.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simu za Mkononi, Sam
Elangalloor, kukagua maeneo ya Shule ya Msingi Kilomo, wakati wa hafla
ya uzinduzi wa shule hiyo, uliofanyika leo shuleni hapo baada ya
kukamilika kwa ukarabati uliofanywa na kampuni ya Simu za mkononi ya
Airtel Tanzania.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simu za
Mkononi, Sam Elangalloor, kuhusu matumizi na makusudio ya mafunzo ya
Kompyuta wakati alipotembelea katika chumba cha Kompyuta, baada ya
kuzindua rasmi shule ya Msingi, Kiromo, leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Sam
Elangalloor, wakati alipokuwa akitembelea katika Chumba cha Maktaba cha
Shule ya Msingi Kilomo, baada ya uzinduzi rasmi wa shule hiyo,
uliofanyika leo.
*****************************
Airtel yaijenga upya Shule ya msingi kiromo kupitia Mradi wake wa ‘Airtel Shule yetu’
Zaidi ya Tsh Milioni 300zatumika kukamilisha ujenzi wa shule Kiromo
Wanafunzi sasa kufurahia mazingira mapya, vifaa vya elimu na sare za shule
Dar es Salaam, Jumanne, Novemba 27, 2012;
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imezindua shule ya msingi kiromo iliyopo bagamoyo mkoa wa pwani baada kuijenga upya shule hiyo nakuipatia vifaa bora vya kufundishia kwa lengo la kutoa mazingira mazuri ya wanafunzi kujisomea.
Ujenzi wa shule ya kiromo ni mwendelezo wa dhamira ya Airtel kupitia mradi wake wa “Airtel shule yetu” wenye lengo la kushirikiana na serikari kuhakikisha wanaweka mazingira bora katika utoaji wa elimu kwa kujenga majengo, kutoa vifaa vya kufundishia pamoja kutoa udhamini wa masomo kwa wanafunzi.
Akizungumza wakati wa halfa ya uzinduzi iliyofanyika shuleni hapo, Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bw, Sam Elangollor alisema “tulianzisha mradi wa Airtel shule yetu kwa lengo la kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha utoaji wa elimu kwa wavulaa na wasichana, tulianza na shule ya Kiromo ikiwa na hali mbaya sana, madarasa yote yalikuwa yameharibika vibaya huku asilimia 80 ya wanafunzi wa umri kati ya miaka 7-13 wakikaa chini.
“Airtel tumerekebisha majengo yaliyokuwepo na kisha kujenga majengo mapya ya madarasa, ofisi kwaajili walimu, maktaba ya shule, darasa la komputa pamoja na jiko kwaajili ya chakula cha mchana kwa wanafunzi” aliongeza bw Ellangaloor .
Vile vile “Airtel tumeweka umeme katika shule hii mara baada ya kuijenga na kuhakikisha tumeweka madawati katika madarasa yote, vitabu vya kutosha katika maktaba, komputa zitakazotumika kwa ajili ya kujifunza somo la kompyuta na kuunganishwa kwenye mtandao wa internet, aliendelea kusema mkurugenzi huyo.
Airtel tunatambua jitihada za serikali yetu katika kuhakikisha inatoa misingi ya elimu bora ili kufikia lengo la Milenia ingawa bado kunachangamoto nyingi katika kutoa elimu bora. Ni imani yetu kupita mradi wetu wa “Airtel shule yetu” tutamuwezesha mtoto wakitanzania kupata elimu bora kwa kuwawekea misingi ya uraia bora na kuchangia katika uchumi wa nchi yetu Alimaliza kusema bw Elangalloor.
Akiongea wakati wa uzinduzi huo mgeni rasmi Mheshimiwa Makamu wa Raisi Ghalib Bilal alifafanua kuwa “Kitu pekee ambacho kinatofautisha nchi zilizoendela na zinazoendelea sio utajiri na mali bali ni elimu. Hii ni kwasababu utajiri na mali havijileti vyenyewe isipokuwa huchochewa na maendeleo mazuri ya msingi wa ELIMU”
hivyo kwakuzingatia hilo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunaishukuru sana Airtel Tanzania kwa kutuunga mkono katika dhamira yetu ya kuwekeza katika sekta ya elimu nchini kwa kujenga na kukarabati shule hii ya Kiromo pamoja na kuwa mstari wa mbele katika kujitolea katika kutoa vitabu kwa shule mbalimbali nchini.
“Napenda kuwashukuru walimu , kamati ya shule, pamoja na wizara ya elimu kwa kushirikiana na Airtel katika kuhakikisha ujenzi wa shule hii umekamilika” aliongeza Mheshimiwa Makamu wa raisi.
Airtel Tanzania imejiwekea mikakati ya kusaidia maendeleo ya jamii hususani elimu ya msingi na sekondari kwa kuwa ndio msingi wa mwanzo kabisa katika mfumo wetu wa elimu.
Kupitia mradi wa “Airtel shule yetu” zaidi ya shule za sekondari 1000 zimefaidika kwa kupatiwa vifaa vya kufundishia vikiwemo vitabu na madawati. Pia Airtel Tanzania inatoa udhamini kwa kulipia gharama za masomo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa wasichana na wavulana ambapo hadi leo hii Airtel inajumla ya wanafunzi watano wanaosoma elimu ya juu kwa kulipiwa gharama zote za masomo huku wengine 34 wameshamaliza na wameajiriwa katika makampuni mbalimbali nchini ikiwemo Airtel.
Mradi wa shule yetu (Adapt the school) ni mpango unaoendeshwa na Airtel katika nchini zote 20 za Afrika.

Yaijengea maktaba pamoja na darasa la kompyuta la kisasa,

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)