Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal (wa tatu kulia) wakati akiwasili
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kumjulia hali Katibu Mkuu wa Mufti wa
Zanzibar, Sheikh Fadhil Soraga aliyemwagiwa tindikali jana huko visiwani
Zanzibar.
Makamu wa Rais na msafara wake wakitoka katika wodi aliyolazwa Sheikh
Soraga.
Makamu wa Rais akiongea na waandishi wa habari katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili baada ya kumjulia hali Sheikh
Soraga.
...Akiingia kwenye gari tayari kwa
safari.
Aliyewahi kuwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Business Times, John
Mapinduzi ambaye hivi sasa ni mwandishi wa habari wa Mhe. Bilal akilifuata gari
tayari kuondoka eneo hilo.
--
MAKAMU
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Gharib Bilal leo amefika
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam kumjulia hali Katibu
Mkuu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Suleiman Soraga aliyenusurika kifo
baada ya kumwagiwa tindikali jana huko visiwani Zanzibar.
Kufuatia tukio hilo, amesema kuwa kitendo alichofanyiwa Sheikh huyo ni cha kinyama na hakitavumiliwa na kwamba serikali inafanya juu chini kuwabaini waliohusika na tukio hilo ili wachukuliwe hatua kali za kisheria.“Hatutavumilia kitendo hicho hata kidogo kwa sababu huu siyo utamaduni wetu tuliojiwekea,” alisema Makamu wa Rais.Jana, Rais Jakaya Kikwete alifika hospitalini hapo kumjulia hali Sheikh Soraga

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)