Hati kuithibitisha
Wilaya ya Kalambo kutoka Mkoa wa Rukwa kuwa mshindi wa kwanza wa shughuli za
mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2012 katika kanda ya nne iliyohusisha Mikoa mitano
ya Kigoma, Katavi, Tabora, Rukwa na Mbeya na Wilaya zake.
Mkuu wa Wilaya mpya
ya Kalambo Moshi Chang'a ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia
Stella Manyanya kwenye shughuli za kuzima Mwenge wa Uhuru Mkoani Shinyanga
akionyesha Kikombe na Cheti alichokabidhiwa na Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete
kama zawadi ya ushindi kwa Wilaya yake baada ya kushika nafasi ya kwanza katika
shughuli za mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2012 katika kanda ya nne
iliyohusisha Mikoa mitano ya Kigoma, Katavi, Tabora, Rukwa na Mbeya na Wilaya
zake alipowasili jana Mkoani Rukwa aikitokea Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya
Sumbawanga Methew Sedoyyeka akimpa Mkono wa pongezi Mkuu wa Wilaya ya Kalambo
Moshi Chang'a kwa ushindi alioupata wa Wilaya yake mpya kuwa mshindi wa kwanza
wa shughuli za mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2012 katika kanda ya nne
iliyohusisha Mikoa mitano ya Kigoma, Katavi, Tabora, Rukwa na Mbeya na Wilaya
zake. Katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed
Chuma.
Katibu Tawala Mkoa wa
Rukwa aikifurahia kikombe hicho.
Ilifanyika tafrija
fupi ya kupongezana kwa ushindi huo wa Wilaya ya Kalambo kwani umekuwa ni
ushindi wa Mkoa mzima wa Rukwa kutokana na ushirikiano uliopo kutoka ngazi ya
Mkoa hadi katika Halmashauri.
Hakika ushindi huo
ulimgusa kila mmoja
Katibu Tawala Mkoa wa
Rukwa ALhaj Salum Mohammed Chima akifurahia kikombe hicho kwa pamoja na
watumishi wenzake.
Katibu Tawala Mkoa
wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akipokea kikombe hicho cha ushindi kutoka
kwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang'a muda mfupi baada ya kumpokea
akitokea Mkoani Shinyanga alipokwenda kumuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwenye
kilele cha kuzima mwenge wa uhuru.
Watumishi Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa Rukwa wakifurahia kikombe hicho cha ushindi.
Wawakilishi wa Mkoa
wa Rukwa waliokwenda kushiriki kuzima mwenge wa uhuru Mkoani Shinyanga na
kurudi na kikombe cha ushindi wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi
Chang'a, mratibu wa Mwenge Kimkoa Abubakar Serungwe na Katibu wa Mkuu wa Mkoan
Frank Mateny wakipewa mapokezi na uongozi na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Rukwa.Picha na Habari zimeletwa hapa na Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)