Mkurugenzi
Mtendaji wa OEDAE Bw. Moeketsi Majoro akisisitiza jambo alipokuwa na
ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Mhe. William Mgimwa, nchini Japan
Tokyo
Waziri wa Fedha Mhe William mgimwa akifafanunua masuala mbalimbali ya uchumi katika mkutano wa IMF nchini Japan Tokyo.
………………………………………………..
Waziri wa Fedha Mhe.Dr. William
Mgimwa amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa kundi namba moja la kanda
ya Afrika anayewakilisha nchi za Afrika kwenye Shirika la Fedha la
kimataifa (IMF) Bw. Moeketsi Majoro.
Hivi karibuni Rais Jakaya Mrisho
Kikwete alimteua Dr. William Mgimwa kuwa Waziri wa Fedha nchini Tanzania
ikiwa ni mara ya kwanza akiwa kama Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki
ya Dunia kuhudhuria Mikutano hii ya Benki ya Dunia na shirika la fedha
la kimataifa inayofanyika hapa nchini Tokyo-Japan. Akiwa katika Mikutano
hiyo, Mgimwa amefanikiwa kuonana na Bw. Moeketsi na kufanya mazungumzo
naye mbalimbali mojawapo likiwa ni jinsi gani Tanzania inaweza kufaidika
na IMF na kuweza kuinua uchumi wake kupitia shirika hilo.
Akizungumza na Bw. Moeketsi,
Mgimwa alisema kuwa, ” Nina mambo muhimu kama manne ambayo ukisaidia
kufikisha ujumbe huu na kama tutafanikiwa kupata fedha hizo tutakuwa
tumepiga hatua sana katika kuinua uchumi wa nchi yetu. Moja, ni
kurekebisha barabara zetu na kuziweka katika viwango vinavyotakiwa,
pili ni mfumuko wa bei, kwakweli mfumuko wa bei umekuwa ukisababishwa na
upandaji wa bei za bidhaa hasa vyakula kama vile mahindi lakini
tumegundua kuwa mchele unapanda sana hata kuzidi mahindi, tatu ni hii
hali ya Tanesco, kwa kweli umeme umekuwa ni tatizo kwetu pamoja na
jitihada zote tunazozifanya na hasa za kutumia gesi.”alieleza Mgimwa.
Aliendelea kusema kuwa tunahitaji
kuimarisha masoko ya ndani na kuwa na dhamana za kutosha, pamoja na
kuwa tumeandaa mipango kamambe ambayo itatusaidia katika kutekeleza haya
lakini bado tunahitaji nguvu kutoka shirika la fedha la kimataifa”.Naye
Bw. Moeketsi alifurahishwa na uelewa wa Mhe. Mgimwa na kumhaidi
kufuatilia kwa karibu, kwani mambo yote aliyoyaeleza ni ya msingi na kwa
sababu yako kwenye mpango mzuri yataweza kutekelezeka. Mazungumzo ya
Mhe. Mgimwa na Bw. Moeketsi yamefungua mianya mipya na mahusiano ya
karibu kati ya na shirika la Fedha la kimataifa na nchi ya Tanzania.
Mkutano huo ulihudhuriwa na
Gavana wa Benki kuu ya Tanzania Bw. Benno Ndulu,Kamishna wa fedha za nje
Bw. Said Magonya, Bi.Mwanaidi Mtanda ambaye ni Mhasibu Mkuu wa
Serikali, Bw.Beda Shallanda ambaye ni Kamishna wa sera, Bi. Monica
Mwamunyanye ambaye ni Kamishna wa Bajeti, Bw. Ahmed Rutashobola ambaye
ni mwakilishi wa Tanzania huko IMF na baadhi ya maafisa kutoka Benki kuu
na Wizara ya fedha .
Aidha Mhe. Mgimwa alimalizia kwa
kueleza kuwa Tanzania imejitahidi sana kupunguza deni la Taifa na
vilevile inafanya jitihada za kuimarisha usimamiaji wa deni hilo kwa
kuhamishia jukumu hilo Wizara ya Fedha ili kuweka usimamizi na udhibiti
wa karibu zaidi.
Nchi za Afrika zimegawanywa katika
makundi matatu na Bw. Moeketsi anaziwakilisha nchi ishirini na moja za
Afrika ambazo ziko kwenye kundi la kwanza.
Imetolewa na Msemaji Mkuu- Wizara ya Fedha
Bi. Ingiahedi Mduma
Tokyo – Japan
08 Oktoba,2012
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)