Na Father Kidevu Blog, Monduli
Mrembo wa Mkoa wa
Manyara, na mwakilishi wa Kanda ya Kaskazini, Lucy Stephano usiku wa kuamkia
leo amenyakua taji la Redds Miss Photogenic 2012 na kuwa mrembo wa kwanza kuingia hatua ya nusu fainali
ya shindano la Redds Miss Tanzania 2012.
Lucy amefanikiwa
kuingia hatua hiyo ambayo itaingiza warembo 15 bora na kuwashinda warembo
wenzake 29 ambao wapo katika kambi ya Redds Miss Tanzania 2012.
Shindano hilo dogo la
Haiba ya Picha “Miss Photogenic” alipatikana
baada ya jopo la majaji ambao ni wapiga picha mashuhuri nchini Tanzania
wakiongozwa na Jaji Mkuu Mroki Mroki.
Mapema akitaja majina
ya warembo walioingia hatua ya tano bora Mroki aliwataja mamaji wengine
aliyoshirikiana nao kuwa ni Mpigapicha Othman Michuzi na Katibu Mkuu wa Kamati
ya Miss Tanzania, Bosco Majaliwa.
Dalili za kuonesha kuwa
Lucy amekubalika hata kwa washiriki wenzake katika shindano hilo ziliibuka
wakati Mroki akitaja majina ya warembo waliofanikiwa kuingia hatua hiyo na
lilipotajwa jina lake ukumbi wa Emanyata uliofurika wakazi wa mji wa Monduli na
warembo ulilipuka kwa kwashangwe.
Warembo watano
walifanikiwa kuingia katika mchujo huo ni pamoja na Magdalena Roy, Lightness Michael,
Babylove Kalala, Diana Hussein na Lucy Stephano.
Warembo wa Redds Miss
Tanzania watashindana tena katika shindano la Miss Top Model linalotaraji
kufanyika Oktoba 13 2012, katika Hotel ya Naura Spring jijini Arusha.
Mataji mengine yatakayo
waniwa na warembo hao na washindi kuingia moja kwa moja klatika hatua ya Nusu
fainali ni Miss Talent, Miss Personality na Miss Sports Woman.
Taji la Miss Photogenic
lilikuwa linashikiliwa na mrembo Stacy Mabula kutoka Shinyanga na Kanda ya
Ziwa.
Fainali za mwaka huu za
Redds Miss Tanzania zinataraji kufanyika katika ukumbi wa Blue Peal Ubungo
jijini Dar es Salaam Novemba 2, 2012.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)