WAZIRI WA FEDHA ATOA CHANGAMOTO KWA MKURUGENZI MTENDAJI WA KANDA YA AFRIKA (IMF) - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WAZIRI WA FEDHA ATOA CHANGAMOTO KWA MKURUGENZI MTENDAJI WA KANDA YA AFRIKA (IMF)

  Mhe. Mgimwa na Mkurungenzi Mtedaji anayeiwakilisha Afrika IMF, akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu Bw. S. Likwilile kwenye mkutano wa IMF  nchini Tokyo-Japan
 Waziri wa Fedha Mhe. William Mgimwa akiwa na wajumbe kutoka Wizara ya Fedha Bi. Monica Mwamunyange  na Bi. Mwanaidi Mtanda Mhasibu Mkuu wa Serikali katika mkutano na Mkurungenzi Mtendaji anayewakilisha Afrika katika Shirika la Fedha la kimataifa  Bw. Moeketsi Majoro Japan- Tokyo
  Waziri wa Fedha Mhe William mgimwa akifafanunua masuala mbalimbali ya uchumi katika mkutano  wa IMF nchini Japan Tokyo.
 Waziri wa Fedha Mhe. William Mgimwa akiwa na ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa IFM nchini Japan-Tokyo
 Mhe. William Mgimwa akiwa na Gavana wa Benki Kuu Benno Ndulu, Mhasibu Mkuu wa serikali B.i Mwanaidi Mtanda na Dr. Massawe wakimsikiliza Mkurungenzi Mtendaji anayeiwakilisha Afrika katika mkutano wa IMF nchini Japan- Tokyo
 Mkurugenzi Mtendaji anayeiwakilisha Afrika katika Shirika la Fedha Bw. Moeketsi Majoro akiwa na ujumbe wake katika mkutano wa IMF nchini Japan- Tokyo.Picha na: Ingiahedi Mduma na Scola Malinga, Tokyo- Japan

WaziriwaFedhaMhe.Dr. William MgimwaakutananaMkurugenziMtendajiwakundinambamoja lakandayaAfrikaanayewakilishanchizaAfrikakwenyeShirika la Fedha la kimataifa (IMF) Bw. MoeketsiMajoro.HivikaribuniRaisJakayaMrishoKikwetealimteua Dr. William Mgimwa kuwa Waziri wa Fedha nchini Tanzania ikiwa ni mara ya kwanza akiwa kama Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki ya Dunia kuhudhuria Mikutano hii ya Benki ya Dunia nashirika la fedhala kimataifa inayofanyika hapa nchini Tokyo-Japan. 

Akiwa katika Mikutano hiyo, Mgimwa amefanikiwa kuonana na Bw. Moeketsi nakufanya mazungumzo naye mbalimbali moj awapo likiwa ni jinsi gani Tanzania inaweza kufaidika na IMF na kuweza kuinua uchumi wake kupitia shirika hilo. 

Akizungumza na Bw. Moeketsi, Mgimwa alisema kuwa,” Nina mambo muhimu kama manne ambayo ukisaidia kufikisha ujumbe huu na kama tutafanikiwa kupata fedha hizo tutakuwa tumepiga hatua sana katika kuinua uchumi wa nchi yetu. 

Moja,nikurekebisha barabara zetu na kuziweka katika viwango vinavyotakiwa,pili ni mfumuko wa bei, kwa kweli mfumuko wa bei umekuwa ukisababishwa na upandaji wa bei za bidhaa hasa vyakula kama vile mahindi lakini tumegundua kuwa mchele unapanda sana hata kuzidi mahindi, tatu ni hii hali yaTanesco, kwa kweli umeme umekuwa ni tatizo kwetu pamoja na jitihada zote tunazozifanya na hasa za kutumia gesi.”alielezaMgimwa. 

Aliendelea kusema kuwa tunahitaji kuimarisha masoko ya ndani na kuwa na dhamana za kutosha,pamoja na kuwa tumeandaa mipango kama mbea mbayo itatusaidia katika kutekeleza haya lakini bado tunahitaji nguvu kutoka shirika la fedha la kimataifa”.

Naye Bw. Moeketsi alifurahishwa na uelewa wa Mhe. Mgimwa na kumhaidi kufuatilia kwa karibu,kwani mambo yote aliyoyaeleza ni ya msingi na kwa sababu yako kwenye mpango mzuri ya taweza kutekelezeka. 

Mazungumzo ya Mhe.Mgimwa na Bw. Moeketsi yamefungua mianya mipya na mahusiano ya karibu kati yana shirika la Fedha la kimataifa na nchi ya Tan zania. Mkutano huo ulihudhuriwa na Gavana wa Benki kuu ya Tanzania Bw. Benno Ndulu, Kamishna wa fedha za njeBw. Said Magonya, Bi.Mwanaidi Mtanda ambaye niMhasibu Mkuu wa Serikali, Bw.Beda Shallanda mbaye niKamishna wa sera, Bi. Monica Mwamunyanye ambaye ni Kamishna wa Bajeti, Bw. Ahmed Rutashobola ambaye ni mwakilishi wa Tanzania huko IMF nabaadhiyamaafisakutokaBenkikuunaWizarayafedha.

AidhaMhe. Mgimwa alimalizia kwa kueleza kuwa Tanzania imejitahidi sana kupunguza deni la Taifa na vilevile inafanya jitihada za kuimarisha usimamiaji wa deni hilo kwa kuhamishia jukumu hilo Wizara yaFedha ilikuweka usimamizi na udhibiti wa karibu zaidi. 

Nchiza Afrika zimegawanywa katika makundi matatu na Bw.Moeketsi anaziwakilisha nchi ishirini na moja zaAfrika ambazo ziko kwenye kundi la kwanza.

Imetolewana
MsemajiMkuu- WizarayaFedha
Bi.IngiahediMduma
Tokyo – Japan
08 Oktoba,2012

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages