Mgeni
rasmi katika uzinduzi wa kijiji cha Maisha Plus Naibu Waziri wa Jinsia,
Wanawake na Watoto Mhe. Ummy Mwalim akitoa hotuba wakati wa uzinduzi
wa shindano hilo kwenye kijiji cha Maisha Plus. Washiriki wa mpango wa mama shujaaa wa chakula unaodhaminiwa na benki ya NMB hatimaye wameingia katika kijiji cha Maisha Plus. NMB inaamini udhamini huo ni
sahihi kutokana na kuwa utakuza kilimo na kuwasaidia wakulima wadogo
katika maisha, mapambano dhidi ya njaa,umasikini na uhaba wa ajira
miongoni mwa wanawake.
Naibu
Waziri wa Jinsia, Wanawake na Watoto Mhe. Ummy Mwalim (kushoto) na
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa Oxfam Bi. Monica Gorman
wakifurahia kinywaji cha dafu wakati wa uzinduzi huo.
Mkurugenzi
wa Shindano la Maisha Plus Bw. Masoud A. Kipanya (kushoto) akijadili
jambo na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NMB, Bw. Imani Kajula (kati)
pamoja na wageni waalikwa katika uzinduzi huo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)