Washiriki wa shindano la The Mic King, waliofuzu kuingia 12 bora kutoka Kinondoni wakiwa kwenye pozi la pamoja.
Kundi la Wakali Dancers likiwajibika stejini.
Majaji wa mchakato huo, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’ (kushoto) na John Dilinga (Dj JD) wakiwa kazini.
Isha Mashauzi akiwarusha roho mashabiki waliohudhuria shoo hiyo ndani ya Dar Live.
Mpiga kinanda maarufu Bongo, Thabit Abdul akitumbuiza jukwaani.Habari/Picha: Musa Mateja/GPL
--
USIKU wa kuamkia leo kulifanyika mchujo mkali wa kuwasaka wakali 12
kutoka Kinondoni wa shindano la The Mic King, ndani ya Ukumbi wa
burudani wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam. Baada ya kumenyana
vikali kwenye steji hiyo huku wakifuatiliwa kwa makini na majaji
wanaoujua muziki vilivyo John Dilinga (Dj JD), na Abdallah Mrisho ‘Abby
Cool’, ambao walifanya upembuzi makini na kuwapata wakali hao ambao ni
Martin Gasper, Jafaar Kassim, Lusajo Kapngala, Peter Lugaman, Emmanuel
Clemence, Ally Zuberi, Abdi Salim, Omary Xavery, Modestus Luiza,
Athuman Ayoub, Dickson Siwalaza na Hudu Juma.
Shindano hilo pia lilisindikizwa na burudani za muziki kutoka kundi la Wakali Dancers na bendi ya Taarab ya Mashauzi Classic.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)