Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw.
Phillippe Poinsot akielezea jinsi shirika hilo linavyoshirikiana na
serikali ya Tanzania katika kufanikisha miradi mbali mbali ya maendeleo
katika kuhakikisha nchi inapiga hatua kwenye kukuza uchumi. Kulia ni
Mwandishi wa Radio France International (RFI Kiswahili) Bw. Ali Bilali.
Mwandishi
wa Habari wa Radio France International (RFI Kiswahili) Bw. Ali Bilali
akifanya mahojiano na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja
wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot (kushoto) ikiwa ni wiki
ya maadhimisho ya miaka 67 ya Umoja wa Mataifa.
…………………………………………….
Na.Mwandishi wetu.
Umoja
wa Mataifa umeanza kuadhimisha wiki mahsusi kwa ajili ya Umoja huo kwa
kufanya shughuli mbalimbali ambapo nchini Tanzania taasisi za Umoja wa
Mataifa, Serikali ya Tanzania na mashirika ya kiraia wanakutana
kuzungumzia maswala mbalimbali yahusuyo maendeleo, utawala bora na njia
za kupiga vita umaskini uliokithiri.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na
Maendeleo nchini Tanzania UNDP Philippe Poinsot, amesema Tanzania ni
nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa ambayo inawajibika vizuri kwenye
umoja huo.
Mbali
na hayo Mkurugenzi huyo wa UNDP amesema kuwa Umoja wa Mataifa
unachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza umasikini uliokithiri nchini
Tanzania ambapo takriban dola za Marekani lakini nne milioni hutolewa
katika kipindi cha miaka minne.
Wiki ya umoja wa mataifa imeanza kuadhishwa Oktoba 17 na itafikia kilele Oktoba 24 mwaka huu.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)