KATIBU MKUU WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA ATEMBELEA RUKWA NA KATAVI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KATIBU MKUU WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA ATEMBELEA RUKWA NA KATAVI

 
NA JOEL MWAKABUNGU  FULLSHANGWE-SUMBAWANGA
Katibu mkuu wa Wizara ya ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Bw.Job Masami alitembelea mikoa ya Katavi na Rukwa kwa ajili ya kutembelea na kukagua maendeleo ya shughuli ya uhamishaji wa shehena ya mahindi kutoka mjini Sumbawanga mkoani Rukwa na kupelekwa mjini Mpanda mkoani Katavi, shughuli inayofanywa na malori yanayomilikiwa na Jeshi la
 
Wananchi wa Tanzania JWTZ. Alielezwa kuwa hadi sasa zaidi ya tani 11,600 za mahindi zimeshahamishwa kutoka Sumbawanga kwenda Mpanda kwa ajili ya kusafirishwa kupelekwa kwenye Kituo cha Wakala wa Hifadhi ya Chakula ya Taifa NFRA cha mkoani Shinyanga, na kwamba ni jumla ya tani 20,000 za mahindi ndizo zinazotakiwa kuhamishwa kutoka 
 
Sumbawanga kwenda Shinyanga kwa ajili ya kukabiliana na suala zima la njaa kwenye maeneo hayo ya kanda ya ziwa. Alipata fursa vile vile kuongea na makamanda wa Jeshi hilo la ulinzi zmbalo lina malori 65 hadi sasa mkoani Rukwa na Katavi yanayohamisha mahindi hayo, na kwamba wana mpango wa kuongeza malori mengine 50 ili kuharakisha uhamishaji wa shehena hiyo ya mahindi, wakilenga kuukimbia msimu wa mvua unaokaribia kuanza, kwani mara kwa mara mvua zinachangia kuharibu miundo mbinu.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages