Kundi zima la The African Stars Band Twanga Pepeta usiku wa ijumaa ya
tarehe 26/10/2012 ndani ya Mzalendo Pub Millennium Towers Kijitonyama
watashambulia katika jukwaa moja na malkia wa mipasho Afrika Mashariki
Bi Hadija Omar Kopa sambamba na mayenu ya nguvu yatakayoporomoshwa na
madj bora nchini,Dj Mackay na Dj Too Short.
Afisa habari wa kampuni ya Mac D Promotions Peter Mwendapole ambao ndio waandaaji wa onyesho hilo la kwanza nala kipekee jijini Dar es salaam amesema maandalizi yote yamekalimika na kinachosubiriwa ni siku yenyewe ifike.
"kila kitu kipo sawa,siku hiyo watu watakaofika watashuhudia burudani bila kikomo,kwani Twanga Pepeta wamejiandaa vyema kuangusha show ya nguvu ikiwa ni pamoja na kuwakumbusha mashabiki wake enzi za shika ungo upepete,kisigino na staili zote walizopata kutamba nazo,wakati malkia wa mipasho Bi Hadija Kopa atazipiga nyimbo zake zote za zamani naza sasa" alisema Peter.
Pia amesema baada ya kuwachezesha Twanga na Kopa,baadaye Dj Too Short na Mackay wataendeleza Fleva Night kwa kuangusha mayenu ya nguvu mpaka jua linachomoza.
Kwa upande wake Bonventure Kilosa "Dj Venture" amesema huu utakuwa usiku wa kipekee kwani wapenzi wa muziki watakaofika ukumbini hapo watapata burudani tatu kwa kiingilio kimoja tu cha shilingi elfu kumi ( 10,000 ) na watakuwa na uhakika wa kukata kiu yao ya burudani kwani kama ni muziki wa dansi utapatikana hapo,muziki wa taarabu hapo na kwa upande wa mayenu ya miaka ile ya akina Mayaula Mayoni,Victoria Ellyson,Dindo Yogo na wengineo siku hiyo zitapigwa non stop mpaka asubuhi.
Kutokana na usiku huu kuwa wa kipekee,afisa huyo habari wa Mac D Promotions Mwendapole amesema suala la ulinzi wa mali na wateja vitaimarishwa. Mpaka sasa onyesho hili limedhamini na SK Bake Palace,na maongezi na wadhamini wengine yanaendelea ili kulifanya liwe onyesho la aina yake.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)