Na Mwandishi Wetu Dar es Salaam
TUME ya Mabadiliko ya Katiba
(kesho jumatatu,terehe8.Oktoba,2012) inatarajia kuanza awamu ya tatu ya
kazi ya ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu KatibaMpya katika Mikoa
tisa (9) ikiwemo saba (7) ya Tanzania Bara na miwili ya Zanzibar.
Taarifa iliyotolewa (leo jumapili
tarehe 7. Oktoba, 2012) Jijini Dar es Salaam, na Katibu wa Tume hiyo,
Assaa Rashid na kusambazwa katika vyombo vya habari inaitaja Mikoa hiyo
kuwa ni Mtwara, Kilimanjaro, Iringa, Singida, Njombe, Rukwa, Tabora,
ambayo yote ni ya Tanzania Bara.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo inasema
pia Tume hiyo inatarajia kuitisha mikutano yake katika mikoa miwili ya
Zanzibar, ambayo ni Kaskazini Unguja na Kaskazini Pemba.
Aidha taarifa hiyo inaongeza kuwa
katika Mkoa wa Mtwara, Tumei taanza na Wilaya ya Nanyumbu, katika Mkoa
wa Kilimanjaro Tume itaanza na Wilaya ya Moshi Mjini, katika Mkoa wa
Iringa Tume itaanza katika Wilaya ya Mufindi. Kwa Mkoa wa Singida, Tume
itaanza na Wilaya ya Iramba, wakati Mkoani Njombe , Tume itaanza na
Wilaya ya Ludewa.
Taarifa hiyo pia inaeleza kuwa
katika Mkoa wa Rukwa Tume itaanzia katika Wilaya ya Nkasi, Mkoa wa
Tabora Tume itaanza katika Wilaya ya Kaliua, Mkoa wa Kaskazini Unguja
Tumeitaanza katika Wilaya ya Kaskazini “A” na Mkoa wa Kaskazini Pemba
Tume itaanza katika Wilaya ya Wete.
Tume hiyo pia inawaomba wananchi
kuhudhuria mikutano itakayoitishwa na Tume na kushiriki kikamilifu
katika kutoa maoni yao binafsi kuhusu Katiba Mpya.
Taarifa hiyo pia inawasisitiza
wananchi wamikoa hiyo hasa wanawake na watu wenye ulemavu kutumia fursa
ya kushiriki katika mikutano hiyo inayoitishwa na Tume ili kutoa maoni
yao kuhusu Katiba Mpya.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)