Shekh mkuu wa Baraza la
Waislamu Tanzania Wilayani Tunduru Alhaji waziri Chilakweche
Rajab Abdalah (17)
--
Na,Steven
Augustino,Tunduru
Watu wanaodhaniwa kuwa ni
Waislamu wenye msimamo Mkali wa Dini wamemvamia na kumpiga Shekh Mkuu wa Baraza
la Waislamau Tanzania Wilayani Tunduru Alhaji waziri Chilakweche na
kumsababishia maumivu makali.
Kabla ya tukio Shekh huyo
alifatwa nyumbani kwake na vijana na kumuomba
watoke nae nje ya eneo la nyumba yake wakidai kuwa wanaomba awasaidie kusuhisha
Mgogoro uliokuwa umezuka katika msikiti wa Kitumbini katika Mtaa huo.
Sambamba na tukio hilo pia kijana
mmoja aliyefahamika kwa jina la Rajab Abdalah (17) Amelazwa katika Hospitali ya
Serikali ya Wilaya ya Tunduru akiwa hajitambui baada ya kushambuliwa kwa
mapanga na watu ambao walidaiwa kukimbilia katika tukio la shambulizi la Shekh
Chilakwechi.
Mashuhuda wa tukio hilo walidai
kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa manane ambapo katika madai yao vijana hao
walimtuhumu Alhaji Chilakwechi kuwa amekuwa akishiriki na kula vyakula vya
wakirsto.
Akiongea kwa taabu alihaji
chilakwechi alidai hakuwa na ubaya nao na wala hajwahi kugombana na mtu hali
ambayo inamshangaza na anaiomba Serikali ifuate mkondo wake kwa
wahusika.
kuhusu tuhuma za yeye kushiriki
katika shughuli za dini katika madhehebu ya wakristo alidai kuwa hicho siyo kitu
cha ajabu kwa viongozi wa dini na kuongeza kuwa wao kama viongozi wa dini huwa
na ushirikiano na huitana na kutembeleana kwa vile dini hailuhusu uhasama
miongoni mwao.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa
Ruvuma Bw. Deusdedth Nsimekli amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza
kuwa jeshji la polisi linaendelea na uchunguzi ili kujua kiini cha tukio
hilo.
Aidha kamanda Nsimeki alikiri pia
kufahamu matukio ya udini yanayo endelea Wilayani Tunduru nakuongeza kuwa jeshi
limejipanga kuhakikisha kuwa wanadhibiti vitendo hivyo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)